FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

Fahamu dalili za mtu mwenye upungufu wa damu

Upungufu wa damu ni tatizo linalosababishwa na kupoteza damu nyingi, kupungua kwa uzalishaji wa chembe hai za da damu na uharibifu wa chembe za damu kutokana na matatizo na magonjwa mbali mbali seli mundu, ujauzito, hedhi nzito, kurithi, magonjwa sugu na Lishe duni yenye ukosefu wa madini ya folic, chuma na vitamini B12.

Dalili zifuatazo zinakuwezesha kutambua kama una tatizo la upungufu wa damu hivyo kukusaidia kuwahi hospitali au kubadili mfumo wa chakula ili kuepuka madhara makubwa ya baadae.

·        Kushindwa kupumua vizuri

·        Vidonda kwenye ulimi au mdomoni

·        Sehemu nyeupe ya jicho kuwa bluu

·        Ngozi kuwa na rangi ya kijivu

·        Kucha kuwa dhaifu

·        Kusikia hasira na kuhamasika haraka

·        Kuchoka sana kuliko kawaida

·        Maumivu makali ya kichwa

·        Kupungua kwa uwezo wa kufikiria

·        Kusikia kichwa chepesi pale unaposimama

·        Miguu na mikono kuwa ya baridi sana

·        Uchovu wa mara kwa mara



Matibabu.
Upungufu wa damu hutibiwa mapema kwa kubadili lishe pamoja na kuongeza lishe yenye vitamini C na B12 pamoja na madini ya Chuma kutokana na visababishi vya tatizo. Mara nyingine vidonge na sindano zenye lishe hizi huweza kutumika hosipitali na matibabu ya tatizo linalosababisha na iwapo mgonjwa yuko katika hali mahututi huweza kuongezewa damu.