Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa mwimbaji wa miondoko ya RnB Chris Brown anatarajia kupata mtoto wa pili na aliyekuwa mpenzi wake mwanamitindo Ammika Harris ambaye aliripotiwa kuwa naye kwenye mahusiano miezi kadhaa iliyopita.
Inaripotiwa kuwa mpenzi wa sasa wa Chris Brown ambaye ni Indyamarie Jean Pelton ameachana na staa huyo baada ya kupata taarifa kuwa Chris amempa ujauzito mpenzi wake wa zamani Ammika huku ikidaiwa kuwa Ammika alionekana mara ya mwisho akiwa na Chris ni January mwaka huu nchini Ufaransa.
Chris Brown na mwanae Royalty
Chris Brown na mwanae Royalty
Chris Brown alibahatika kupata mtoto wa kike ambaye ni Royalty ambapo alizaliwa May 27,2014 na mwanadada Nia Guzman mwenye uraia wa Brazil.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)