FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

BABA MATATANI KWA KUMBAKA NA KUMLAWITI BINTI YAKE

Mahakama ya Wilaya ya Temeke imemsomea maelezo ya awali mshtakiwa Haruna Abdu(54) mkazi wa Mbagala Mwanamtoti kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti binti yake wa kumzaa(12)
Mwendesha mashtaka amesema kuanzia Januari 2017 hadi Februari 2019 mshtakiwa alikuwa akimbaka mwanaye huyo wa kumzaa na kumuingilia kinyume na maumbile na ilipofika Februari 2019, mtoto huyo alishindwa kwenda shule kutokana na vitendo alivyofanyiwa
Alisema alipohojiwa na mwalimu wake aliyefahamika kwa jina la Ngulula, mtoto huyo alimueleza kuwa alikuwa anafanyiwa vitendo hivyo na baba yake ndipo taarifa ilipotolewa kituo cha Polisi na mshtakiwa kukamatwa
Hata hivyo, mshtakiwa alikana shtaka mbele ya Mahakama