FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

MWANAFUNZI AMUUWA MWENZAKE KWA KUMPIGA JIWE KICHWANI

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Rashid Said (17) amefariki dunia baada ya kudaiwa kupigwa jiwe lililompata kichwani eneo la kisogoni na mwenzake ambae ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Nyumbu huko Kibaha mkoani Pwani. 
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa amesema kuwa tayari jeshi la Polisi linamshikilia mwanafunzi huyo ili kuendelea na taratibu za kisheria. 
Alieleza kuwa Juni 7 mwaka huu maeneo ya Pichandege marehemu alijeruhiwa kwa kupigwa jiwe baada ya tukio hilo alipelekwa katika hospital ya rufaa ya Tumbi kwa matibabu ambapo siku iliyofuata alifariki dunia. 
Mwili wa marehemu umepelekwa hospital ya taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi. Jeshi la polisi Pwani limetoa wito kwa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi ili kujiepusha na matatizo ama kujikuta wakichukuliwa hatua za kisheria.