FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

SIMBA YAKATA KIU YA MASHABIKI WAKE


Dar es Salaam. Bao la kiungo Mohamed Ibrahimu limetosha kuipamba Simba Day kwa wenyeji Simba kushinda bao1-0 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda kwenye Uwanja wa Taifa.

Ushindi huo umekuwa ni faraja kubwa kwa mashabiki wa Simba waliofuriki uwanjani hapo wakati wa kushudia wachezaji wao wapya wakitambuliwa.
Kiungo Mo Ibrahimu aliwainua mashabiki wa Simba katika dakika ya 16, akimalizia pasi ya Emmanuel Okwi.

 Bao hilo lilitokana na pasi fupi walizopigiana James Kotei, Muzamiru Yassin na Okwi kabla ya kuupeleka mpira kwa Ibrahim aliyepiga shuti la chini chini lililomshinda kipa wa Rayon na kujaa wavuni.

Viungo washambuliaji wa Simba waliocheza nyuma ya John Bocco walicheza kwa maelewano mazuri ya uchezaji kuanzia kwenye namna ya kubadilishana nafasi mara kadhaa Okwi amekuwa akihama upande wa kushoto na kuja kucheza nyuma ya Bocco wakati huo Ibrahimu naye akienda upande aliotoka Okwi vivyo hivyo na upande wa Kichuya na kuwapa wakati mgumu mabeki wa Rayon katika kuwazuia.

Pamoja na bao hilo la Mo Ibrahimu shangwe na furaha za mashabiki wa Simba zilipamba zaidi wakati kiungo wao Haruna Niyonzima aliyesajiliwa kutoka Yanga alipoingia katika kipindi cha pili.

Katika kipindi hicho kocha wa Simba, Joseph Omog aliwaingiza mshambuliaji Mghana Nicholas Gyan,  Niyonzima, Jonas Mkude na Ally Shomary wakichukua nafasi za Jamal Mwambeleko, James Kotei, Mohammed Ibrahim na Okwi.

Simba wamefanya mashambulizi ya mfululizo langoni mwa Rayon kuanzia dakika ya 61, 62 na 63.  Dakika ya 61, Bocco anapewa pasi nzuri na Gyan, lakini shuti lake linaokolewa na kuwa kona ambayo inaokolewa na kunaswa na Muzamiru anayempasia Niyonzima aliyepiga naye anapiga pasi ya kisigino kwa Kichuya dakika ya 62 ambaye shuti lake naye linaokolewa na kipa Mutuyimana Evariste.

Zungu aipa tano kamati ya usajili Simba
 Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu ametoa pongezi za kipekee kwa kamati ya usajili ya Simba kwa kusuka kikosi kizuri msimu huu.
Simba ilionekana kwa mara ya kwanza jijini Dar katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.

Zungu alisema timu hiyo ina kila aababu ya kutamba msimu ujao.
Naiona Simba ya tofauti wana wachezaji wengi wazoefu na wapambanaji. Hiki ndio kitu muhimu katika soka,"alieleza  Zungu.

Mbunge huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa Bunge alisema Simba pia itatamba kwenye mashindano ya kimataifa mwakani.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema huenda uongozi ukaipeleka timu Zanzibar.