Simba yaaga mashindano SportPesa
Katika mchezo huo Simba iliwatumia wachezaji wake wengi wapya ilitegeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini washambuliaji wake walikosa umakini katika umaliziaji.
Kuondolewa kwa Simba kunaifanya Yanga kuwa mwakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano hayo ya kusaka kucheza na Everton dhidi ya timu tatu za Kenya ambazo ni Gor Mahia, AFC Leopards na Nakuru zilizofuzu kwa nusu fainali.
Ndoto ya Simba kucheza nusu fainali ilipotea baada ya kipa Daniel Agyei kukosa penalti ya pili, ikiwa ni penalti pekee waliyopoteza.
Penalti za Simba zilifungwa na Besala Bokungu, Mwinyi Kazimoto, Hafidh Mussa na Finton Murenezo.
Kocha wa Nakuru, Maina George alisema timu yake ilipambana vikali na kufanikiwa kupata matokeo hayo.