FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

Serikali ya Libya yapinga kuachiliwa mwana wa Gaddafi, Seif Al Islam






Serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini Libya, imepinga kuachiliwa kwa mwana wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Kanali Gaddafi.
Seif Al Islam Gaddafi, alikuwa amezuiliwa na kundi la wanamgambo katika mji ulio magharibi wa Zintan.
Amekaa gerezani kwa muda wa miaka 6 kufuatia mapinduzi yaliyomundoa madarakani babake mwaka 2011, na aliachiliwa baada ya kupewa msamaha.
Kuachiliwa kwa Bwana Al Seif Al Islam huenda kukazua msukosuko zaidi katika nchi hiyo ambayo tayari imegawanyika.
Kwa wale waliokusanyika Tripoli miaka 6 iliyopita kuitisha uhuru, itakuwa ni kama hujuma kwao.
Lakini wengi wa wale waliohojiwa mjini Tripoli walikaribisha kuachiliwa kwa Seif Al islam



Hili halijakuwa jambo la kushangaza hasa kutokana na ghasia ambazo zimeshuhudiwa tangu babake apinduliwe.
Mwanamke mmoja alisema kuwa wale waliokuja baada ya kanali Gaddafi, wamesababisha madhara makubwa nchini Libya na mwanawe anaweza kuleta udhabiti.
Wafuasi wake watakuwa na matumaini kuwa atarejea siasa, lakini bado ni mtu anayetafuwa, akituhumiwa kwa uhalifu wa kivita na mahaka ya kimataifa ya ICC.
Alikamatwa jangwani mwezi Novemba mwaka 2011 alipojaribu kukimbia kuenda Niger.
Mwaka 2015 alihukumiwa kifo na mahakama ya mjini Tripoli kwa kufanya uhalifu wakati wa mapinduzi ya babake.

Na bado anatafutwa na mahakama ya ICC mjini Hague, kwa mashtaka yanayohusu uhalifu dhidi ya binadamu.
Seif, ambaye alikuwa mpenda anasa alionekana kama mrithi wa utawala wa babake.