FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

Vyuo vikuu bora zaidi duniani mwaka 2017





Orodha mpya ya kila mwaka ya vyuo vikuu bora zaidi duniani imetangazwa, ambapo chuo kikuu cha Massachusetts Institute of Technology (MIT) cha Marekani bado kinaongoza.
Vyuo vikuu vya Stanford na Harvard - pia kutoka Marekani - kadhalika vimeendelea kushikilia nafasi ya pili na ya tatu mtawalia.
Orodha hiyo ilishirikisha vyuo vikuu karibu 1,000.
Vyuo vikuu hupimwa kwa mambo kama vile majarida na vitabu vya kisomi vilivyochapishwa, makala zilizonukuliwa, maoni ya wasomi pamoja na waajiri na pia ushiriki wa vyuo vikuu hivyo katika ngazi ya kimataifa.
Chuo kikuu cha Nairobi kimeorodheshwa kuwa kati ya nambari 801 na nambari 1000, kutoka kuanzia nambari 701 hadi 1000mwaka jana, sawa na Chuo Kikuu cha Makerere.

Vyuo vikuu 10 bora zaidi
duniani kwa mujibu wa QS World University Rankings
  1. Massachusetts Institute of Technology (MIT)
  2. Stanford
  3. Harvard
  4. California Institute of Technology (Caltech)
  5. Cambridge
  6. Oxford
  7. University College London
  8. Imperial College London
  9. Chicago
  10. ETH Zurich