FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

SAMIA ATALAJIA KUFANYA MAGEUZI YA KILIMO NCHINI

 


 Samia Suluhu wapili kushoto akifungua mirandi
                   mbambali juzi mkoani Kagera akiwa  katika ziara ya siku tatu


Na Kalebo Mussa

Rais Samia Suluhu amezidua kiwanda cha Sukari cha Kagera na mradi wa maji wa Kyaka Bunazi wenye thamani ya bilioni 15.7 kwa fedha za ndani ambao utatoa lita milioni 8 kwasiku ambapo utanufaisha kaya 1000 sawa na watu 35,000 mkoani Kagera.  

Akizungumza jana Mkoani Kagera katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya ujenzi wa mitambo wa kuzalisha umeme kiwanda cha Sukari cha Kagera alisema kutokana na kilimo kuchangia asilimia 58 ya kipato cha nchi Serikali itatekeleza sera yake ya kiuchumi shirikishi kwa kuihusisha sekta binafisi kama mdau  mkuu katika kuleta mageuzi ya kilimo cha kisasa.

 “Ziara hii ni  mfano wa kuleta  mageuzi ya kilimo, nimeona mashaba makubwa ya miwa ndani ya kiwanda cha Sukari cha Kagera, nimeona kazi kubwa inayofanywa kuanzia uwekezaji uliofanywa kwa mitambo ya kisasa , pia nimeshuhudia miundombinu ya umwangiliaji kwa kuweka mambo kwa zaidi ya kilomita 400 na station za kusukuma maji zenye pampu kubwa,” alisema  Samia.  

Alisema huu ni mfano wa kuigwa kuwa na kilimo cha kisasa nchini ambao uliofanywa na wazalendo na kuchangia kuwapatia vijana ajira  ambao wamehitimu vyuo mbambali nchini.

“Niseme ukweli nimevutiwa sana na ajira niliyokuta hapa nimekuta vijana wengi waliohitimu vyuo mbalimbali wako hapa wanafanya kazi kwa weledi mkubwa wanafanya mambo makubwa” alisema Samia.  

Samia alisema katika uzalishaji wa Sukari katika miaka ya 2020 na kuendelea kutakuwa na ongezeko kubwa la kilimo cha miwa hali kadhali itaendana na utanuzi wa viwanda kila sehemu ambapo itakuwa nifaraja kubwa kwa uchumi wanchi na kuwa na Sukari ykujitosheleza.

Alisema watu wa fedha washushe liba kwaajili ya kuimalisha zaidi sekta ya ukewaziji katika maeneo mbalimbali  nchini.

“Watu wa fedha nawashukuru mmeshusha liba kutoka mlipokuwa kwa shiling mpaka sasa mpo aslimia 9 ambapo ni kwa CRDB ila wengine bado mko juu kwenye asilimia 10 kwahiyo tunawaomba mwenedele kushusha zaidi, mnavyoshusha kwenye shilingi pia mshushe kwenye dola kwani uwekezaji huu ni wa dola kuliko shilings” alisema Samia .

Aliongeza kuwa kupitia Benki Kuu ya Tanzania BOT Serikali itaangalia sekta ya kilimo kupunguza liba kwani itakuwa raisi kuwa na uwekezaji mkubwa.  

Kwaupande mwingine Samia alisema ili tuwe na mafuta yakula ya kujitosheleza ni lazima kama taifa tuwe na kilimo ili tufanye uzalishaji wa ndani tuache kutegemea kwa kiasi kikubwa nje.

“Ili tujitosheleze kwenye mafuta ya kula lazima tuwe na mashamba makubwa kutokana na Kagera kuwa na mashamba makubwa yatumike kwaajili ya kuzalisha bidhaa hii muhimu kwa Watanzania” alisema Samia.

Serikali imetengea bilioni 20 kwaajili ya kilimo nia ikiwa ni kuzalisha mafuta ya kula ndani ambayo itakuwa ni suluhusho la upandaji bei wa mafuta ya kula

Samia aliwapongeza wawekezaji .wote kwa uwekezaji endelevu katika sekta zote nchini ambao unaleta tija kubwa kwa Watanzania wengi.

Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda cha Sukari Kagera Bw, Seif Seif alisema mageuzi yavitendo ya kilimo yanaenda kufanyika kwa kuongeza ajira na uzalishaji wa Sukari inayotosheleza nchini.

“Sisi wazalishaji wa viwanda vya sukari tumeshudia juhudi na mipangao thabiti ya sekta binafi kuongeza uzalishaji ili kufanyikisha azima ya kuzalisha Sukari inayotosheleza mahitaji ya nchi yetu na kuuza Sukari ya ziada katika masoko ya nje,” alisema Seif.

Alisema kukamilka kwa daraja linalounganisha Wilaya ya Misenyi na Kalagwe limeleta faraja kubwa kwa kiwanda cha Sukari cha Kagera kufanyika kilimo cha miwa wilayani Kalagwe na fursa za ajira.

Naye, Waziri. Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji alisema Serikali imeanza kuongea na wawekezaji waanze kuzalisha sukari ya dani, watoe ajira kwa watanznia

“Imani yetu kama Serikali nikuwa kiwanda cha sukari cha Kagera kitaendelea kutoa ajira kwa watanznia na kuzalisha sukari kwa wingi ambayo itatosheleza nchini” alisema Kijaji

Aidha ,  Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe alisema mpaka sasa nchi inaagiza kuagiza mbegu mbalimbali za kilimo na kuleta pembejeo kwa ajili ya wakulima ili  kuzalisha mazao mbambali ambayo yatainufaisha taifa.

“Serikali katika kuhakikisha inaongeza tija imejipaga kuleta mapinduzi ya kilimo kwa kuzalisha mazao mbalimbali vilevile viwanda kupitia wawekezaji wazidi kuzalisha Sukari kwa wingi lengo ikiwa ni kuwa Sukari yakutosha nchni” alisema Bashe.