FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

DIAMOND PLATNUMZ AUNGA MKONO KAMPENI YA BONGE LA MPAMBANAJI




Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga amezindua kampeni ya ‘Bonge la Mpambanaji’ ambayo ni maalum kwa ajili ya kuwawezesha Wahudumu wa Afya Tanzania kwa vifaa tiba na mahitaji mengine kwenye vita hii dhidi ya kirusi corona.

Wakati akihojiwa na Power Breakfast ya Clouds FM Kusaga 
akasema anao Wapambanaji wenzake ambao wako tayari kuungana na yeye na miongoni mwao ni Vodacom, Tigo na Diamond Platnumz ambaye alimpigia simu ‘LIVE’ na kuzungumza kwenye Power Breakfast.

Akiongea kwenye ‘PB’ Diamond alisema “Kwanza nimpongeze C.E.O Kusaga kwa kuweka nguvu zake kwenye hilo sio kila Mtu mwenye moyo huo, mimi pia nitaweka mchango wangu hapo na kama unavyofahamu tayari pia upande wangu nimeanza kulipia kodi familia zilizokwama kutokana na hii corona”

Baada ya kuzungumzia Bonge la Mpambanaji, CEO Kusaga alimtaka Diamond achague wimbo wake ili uchezwe kwenye PB kuwaamsha Wapambanaji wote ambapo mara ya kwanza alipendekeza apigwe msanii wake mpya zuchu lakini baada ya mkurugezi huyo  kusisitiza kuwa ngoma ya Diamond ndiyo inatakiwa, Platnumz alichagua yope remix na ikapigwa via Clouds FM kupitia kipindi cha Power Breakfast

Hata hivyo hali hii imekuja kwa tofauti sana kwa baadhi ya mashabiki ambapo baadhi yao walitoa maoni yao juu ya msanii huyo kuunga mkono katika kampeni hiyo.  

“Hiki kitu binafsi nakitamani maisha yangu yote,natamani isiwe leo tu i wish siku zote ngoma za wasafi zipigwe Clouds,hata kama kuna makando makando mengine huu ni wakati wa ushirikiano kati ya Wasafi na Clouds fm,hivi mushawai kuwaza kama kuna vitu vitafanyika kwa ushrikiano kati hizi kampuni 2 hapa bongo kuna moto mkubwa sana utawaka kwenye tasnia hiyo?” aliandika moja ya mashabiki.


ROSE NDAUKA AWAJIBU WATU HAYA
  



 Msanii wa Bongo Movies, Rosse Ndauka amefunguka mara baada ya maswali kuwa mengi kuhusu yeye kubadili dini.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka wazi jambo hilo  kwa kuwata watu waache kujifanya kuwa wanajua mambo mengi kuliko uhalisia wenyewe  

“Maswali yamekuwa mengi sana kuhusu kubadili dini, haya ni hivi nimetoka kwenye tumbo la mwanamke wa kiislam na kulelewa na mwanamke huyu kwakifupi nimekuwa kwenye Uislam na baba akiwa christian, Naveen ni Muslim kabisaaaa bila kupepesa sasa jamaniii acheni kutaka kujua sana mengine tuwaachieni wenyewe,” aliandika  Rose Ndauka.

Hili limekuja mara baada ya Rose Ndauka kufunga ndoa ya Kiislam hivi karibuni na mchumba wake wa siku nyingi ikiwa ni miezi michache tangu kuvishwa pete ya uchumba.



DAVIDO AWATOLEA POVU MASHABIKI WA WIZKID




Msanii kutoka nchini Nigeria David Adedeji Adeleke ‘Davido’ ameonesha  kuchukizwa na mashabiki wa Wizkid, awajia juu hii ni baada yakuweka wazi ujio wa Kolabo yake na Nicki Minaj.

Kupitia twitter, mashabiki hao kindakindaki wa Wizkid walianza kumbeza Davido kwa kumwambia "Kama ingekuwa Wizkid, basi Nicki Minaj ndio angekuwa na wenge la ku-tweet kuhusu hii Kolabo na kuitangaza, lakini sio kama ambavyo Davido amefanya. OBO inatakiwa awe mpole." aliandika shabiki mmoja wa Wizkid.

Baada ya hapo haikumchukua hata dakika Davido ambaye aliibuka na kujibu tweet hiyo kwa kusema ana mpenda Wizkid na kumalizia na matusi mazito.


 NAJ AMKINGIA KIFUA BARAKA DA PRINCE 





Mpenzi  wa msanii wa Bongo Fleva Baraka Da Prince, Najdattani amtetea mpenzi wake huyo kwakile kinachodaiwa kuwa anaongoza kuwajibu vibaya mashabiki kupitia mtandao wa Instagram.

Akilifafanua suala hilo Naj alisema kuwa sasa hivi amejitafuta na amebadilika kwa kutowajibu watu vibaya katika mtandao wa Instagram.

“Kiukweli amelifanyia kazi hilo jambo, sidhani kama kipindi cha hapa karibuni amemjibu mtu vibaya kuna muda inatokea kama binadamu, kuna comments zinakukwaza sana hadi ukapoteza muelekeo, huyu sio Barakah yule ambaye mmemzoea kwamba kila kitu kinamkasirisha ndiyo maana amejitafuta kwenye hiyo miaka miwili". Alisema Baraka

Ikumbukwe kwamba hili limekuja mara baada ya kuwepo kwa  taarifa juu ya kutajwa kuwa mpenzi wake huyo ndiye msanii anayeongoza  kuwajibu vibaya mashabiki mitandaoni.