FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

Pacha walioshikana wafariki hospitalini Tanzania




Pacha walioshikana ambao walikuwa wamelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili mjini Dar es Salaam wamefariki kwa mujibu wa msemaji wa hospitali hiyo.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, pacha hao waliokuwa wakifanyiwa vipimo ili kuwaanda kwa upasuaji walifariki siku ya Jumanne kulingana na bi Neema Mwangomo.
Watoto hao walizaliwa wilayani Kilosa katika eneo la Morogoro.
Familia yao ilitoka katika kijiji cha Chaumbele.
Akizungumza na gazeti la The Citizen, Bi Mwangomo alisema kuwa wataalam watatoa maelezo katika wakati ufaao.
Pacha hao walioshikana chini ya kifua na tumboni walikuwa wakitumia ini moja na mishipa ya moyo lakini kila mmoja alikuwa na tumbo lake.
Awali daktari wa watoto Dkt Zaituni Bokhary alitumai kwamba pacha hao wanaweza kutenganishwa watakapofikisha umri wa miaka sita.