Mechi za Kirafiki za kimataifa kwa mujibu wa Kalenda ya FIFA zinaendelea tena hii leo Jumanne kwa Mechi kadhaa ambapo Australia wanakabiliana na Brazil na Ufaransa kuivaa England.
Argentina wao watakuwa huko Singapore kuwavaa Wenyeji wao Singapore, Indonesia wanawakaribisha Puerto Rico ,Afrika kusini ni wenyeji wa Zambia, Norway watachuana na Sweden, Romania dhidi ya Chile, Cameroon wanacheza na Colombia.