Rais wa Marekani Donald Trump
ameutaja utawala wa taifa la Korea Kaskazini kuwa wa kikatili kufuatia
kifo cha mwanafunzi mmoja wa Marekani ambaye alikuwa amefungwa jela kwa
zaidi ya miezi 15 nchini humo.
Korea Kaskazini ilimrudisha
nyumbani Marekani, Otto Warmbier mwenye umri wa miaka 22 wiki iliopita
ikisema kuwa alikuwa hana fahamu kwa kipindi cha mwaka mmoja na kwamba
ilikuwa ikimsaidia kibinaadamu.Wazazi wake wanasema kuwa aliteswa vibaya.
Bwana Warmbier ambaye alifungwa kwa kujaribu kuiba bango la propaganda kutoka kwa hoteli moja hakuweza kupata fahamu tena.
Bwana Warmbier ambaye alifungwa kwa kujaribu kuiba bango la propaganda kutoka kwa hoteli moja hakuweza kupata fahamu tena.
Wanasema kwamba wakati Otto aliporudi Cincinnati alikuwa hawezi kuzungumza na hakuweza kuona.