Wapinzani wakiandamana nchin DRC CONGO
Umoja wa mataifa umetoa wito ya
kuachiwa mara moja kwa watu 30, wa chama kikuu cha upinzani katika
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kutoka korokoroni.
Utawala wa Rais, Joseph Kabila, umepiga marufuku mkutano wa aina yoyote wa kisiasa, pamoja na maandamano ya upinzani, tangu muda wake wa kuhudumu kama Rais kisheri, ulipomalizika mwaka mmoja uliopita.
Rais Joseph Kabila amesalia mamlakani hata baada ya muhula wake kudumu kumalizika mwaka uliopita
Tume ya uchaguzi nchini humo, imesema kuwa, haitakuwa rahisi kuandaa uchaguzi mkuu wa Urais, kabla ya mwezi Aprili mwaka ujao wa 2019.
Chama kingine cha upinzani- Union for the Congolese Nation, kimesema kwamba, kitajiondoa katika serikali ya ugawanaji mamlaka, kuhusiana na kucheleweshwa kwa uchaguzi mkuu.
Maandamano ya mara kwa mara ya upinzani nchini humo umekabiliwa vikali na utawala wa Rais Joseph Kabila.