Watu nane wanasadikiwa kuvamia na kuvunja jengo la Prime House lililopo mtaa wa Tambaza eneo la Upanga karibu na ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) usiku wabkuamkia leo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amrthibitisha kuvamiwa na kuvunjwa kwa jengo hilo lenye ofisi mbalimbali ikiwamo ofisi ya Mawakili wa Prime Lawyers. Akizungumzia tukio hilo mmoja wa mawakili wa Prime Lawyers amedai kwamba mlinzi wa jengo hilo amekutwa amefungwa kamba miguuni na mikononi pamoja na mdomo kwa kutumia plasta.
"Kwa sasa ni mapema sana kujua ofisi gani zilizoathirika kwenye uvamizi uliotokea, polisi wanaendelea na uchunguz kujua nini kilichotokea," ameeleza wakili huyo. Akizunhumza kwa njia ya simu asubuhi, Kamanda Hamduni amesema Polisibwako eneo la tukio kwa uchunguzi wa awali ili kujua ofisi zilizoathirika kutokana na tukio hilona kusudio la wavamizi hao.