Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), umeanza asubuhi hii mjini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine mkutano huo pia utafanya uchaguzi wa viongozi wa kuongoza taasisi hiyo kubwa inayosimamia mpira wa miguu mchini.
Miongoni mwa watakaochagukiwa hii leo ni pamoja na Rais wa TFF, Makamu wa Rais pamoja na wajumbe wa Shirikisho hilo. Wagombea katika nafasi ya Urais ni pamoja na Ally Mayay, Shija Richard, Wallace Karia, Emmanuel Kimbe, Fredrick Mwakalebela na Imani Madega.