Melania Trump na mtoto wale wamehamia Ikulu ya Marekani ya White House miezi mitano tangu mumewe Donald Trump kuingia ofisini
Bi Trump na mtoto wake kiume wa umri wa miaka 11 Baron, walikuwa wamebaki mjini New York ili kumuwezesha kumaliza masomo ya mwaka.
Hatua hiyo imekuwa ya kushangaza kwa wengi kwa kuwa ndiyo familia ya kwanza miaka ya hivi karibuni kukosa kuhamia Ikulu ya White House mara moja.
Mtangulizi wake Michelle Obama hata alhamia White House, mapema kuwezesha watoto wake kujunga na shule mapema.
Hata hivyo inaonekana kuwa Melania amefurahishwa na hatua yake kuhamia White House baada ya kuandika kwenye Twitter alipowasili.
Barron amekuwa akisomea shule ya kibinafsi iliyopo jiji la New York.
Trump si rais wa kwanza wa Marekani hivi karibuni kuhamia White House akiwa na watoto wa umri wa kwenda shule.
Rais Barack Obama alipoingia madarakani, mabinti wake Malia na Sasha walikuwa na umri wa miaka 10 na 7.
Rais Bill Clinton alipohamia ikulu Washington, Chelsea Clinton alikuwa na miaka 12.
Watoto hao wote walihamia White House masomo ya kiendelea na walihudhuria masomo shule ya Sidwell Friends, shule ya kibinafsi iliyo kaskazini magharibi mwa Washington.