Polisi nchini
Australia imemshitaki kadinali wa kanisa katholiki mwenye ushawishi
mkubwa George Pell, kwa makosa kadhaa ya kuwanyanyasa watoto kingono.
Kadinali Pell amekanusha makosa hayo ambayo yanasemekana kufanyika miaka ya 1970.
Anatarajiwa kufika mbele ya mahakama ya Melbourne mwezi Julai.
Waakilishi wa kanisa hilo hata hivyo hawajatoa tamko lolote juu ya swala hilo licha ya BBC kutoa ombi la kuwataka kufanya hivyo.
Idara
ya Polisi, iliamua kuchukua hatua ya kumfungulia mashtaka Kadinali
Pell, baada ya kupata ushauri kutoka kwa viongozi wa mashtaka mwezi
uliyopita.
Naibu kamishena wa polisi amesema mchakato wa kumfungulia mashtaka kadinali huyo, haina tofauti yoyote na uchunguzi wowote.
Kadinali Pell ni mweka hazina wa Vatican na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki nchini Australia
Mashtaka hayo yanatokana na madai ya ''kihistoria'' ,maafisa wa polisi katika jimbo la Victoria wamesema.
Madai hayo yalitolewa zaidi ya mtu mmoja ,alisema naibu wa kamishna wa polisi Shane Patton.
Kadinali Pell ambaye makao yake makuu yako Vatican amekana madai hayo.
Akiwa mweka hazina wa Vatican kadinali Pell anatambulika kuwa afisa wa tatu mkuu katika kanisa katoliki.Kadinali
Pell atarudi nchini Australia kwa haraka iwezekanavyo ili kujisafishia
jina lake kufuatia ushauri ulioungwa mkono na madktari wake ambao pia
watamshauri kuhusu mipango yake ya kusafiri ,kanisa hilo lilisema katika
taarifa siku ya Alhamisi.
Alisema kuwa yuko tayari kufika mahakamani na atatetea mashtaka yanayomkabili.
Kadinali
huyo sio mkuu wa kanisa katoliki nchini Australia bali pia ni miongoni
mwa viongozi wakuu walio na hadhi ya juu katika ulimwengu wa kanisa
hilo.
Katika kipindi cha miongo miwili amekuwa amekuwa katika
mstari wa mbele katika mjadala wa kanisa hilo kuhusu maswala tata kama
vile lile la wapenzi wa jinsia moija ,ukimwi na utafiti wa seli.
Pia amehusika katika kutoa majibu ya kanisa hilo kuhusiana na madaia ya unyanyasaji wa kingono nchini Australia.