FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

LUKA MODRIC AMEKUBALI KUONGEZWA KANDARASI

 



                                                                   Luka Modric

Kama inavyofahamika Luke Modric ambaye anacheza katika klabu ya Real Madrid ameongeza kadarasa ya kuendelea kusalia hapo mara baada ya  klabu hiyo kumpa mkataba mpya.

Kutokana na ripoti iliyolipotiwa na AS ilisema kuwa Modric amekubali kuongeza muda wake wa kukaa hadi 2023, huku kukiwa na chaguo la miezi 12 zaidi iwapo ataendelea kufanya vizuri.

Modric iwapo atasalia Real Madrid hadi 2024, atakuwa chini ya miezi mitatu kabla ya kutimiza miaka 39, ingawa hapo awali alitaja uwezekano wa kucheza hadi atakapofikisha miaka 40.

Modric amefurahia maisha mazuri tangu alipohamia Uhispania, akishinda Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia la Vilabu mara nne mfululizo.

Pia ametwaa mataji mawili ya LaLiga, na vijana wa Carlo Ancelotti watatwaa ubingwa mwingine iwapo watapata pointi kutoka kwa mechi yao ya nyumbani dhidi ya Espanyol Jumamosi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 amemulika katika michuano ya kimataifa pia, akiwa nahodha wa Croatia hadi fainali ya Kombe la Dunia mwaka wa 2018.

 Aidha, Modri bado hajaonyesha dalili zozote za kupunguza kasi yake, na kutoa pasi nzuri ya mabao na kuisaidia Real Madrid katika mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Chelsea.

Hata hivyo, miamba hao wa Uhispania walijikuta wakiwa nyuma kwa mabao 4-3 baada ya mechi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Manchester City, lakini Modric anatumai kurekebisha kasoro hii kwenye mechi ya marudiano kwenye Uwanja wa Bernabeu siku ya Jumatano akienda kutafuta Mabingwa wake wa tano.