FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

HII HAPA RATIBA YA EPL 2019/2020 MAN U KUANZA NA CHELSEA


MABINGWA  wa Ligi Kuu England, Manchester City wataanza kutetea ubingwa wao dhidi ya West Ham wakati Manchester United itafungua ligi dhidi ya Chelsea Agosti 11 katika msimu wa 2019-20.

Katika ratiba hiyo ya Ligi Kuu England iliyotolewa leo inaonyesha mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Liverpool,  watafungua msimu nyumbani dhidi ya timu iliyopanda daraja la Norwich City hapo Ijumaa ya Agosti 9, siku ambayo ligi hiyo itaanza rasmi.



Mabingwa Manchester City watakuwa ugenini Agosti 10 kuifuata West Ham. Timu zilizopanda daraja za Aston Villa na Sheffield United watakata utepe kwa kucheza dhidi ya Tottenham na Bournemouth ambapo Jumapili ya Agosti 11, Manchester United watakuwa nyumbani kuwakaribisha Chelsea.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Ligi Kuu England, klabu zitapata mapumziko mafupi ya wiki mbili mwezi Februari.

Mapumziko hayo katika wiki ya kwanza kutakuwa na mechi tano na wiki ya pili mechi tano ili kuhakikisha kila klabu inapata wiki moja ya kupumzika.



Ratiba ya ufunguzi
9 Agosti 2019 Liverpool v Norwich City
10 Agosti 2019 West Ham v Manchester City
10 Agosti 2019 Bournemouth v Sheffield United
10 Agosti 2019 Burnley v Southampton
10 Agosti 2019 Crystal Palace v Everton
10 Agosti 2019 Leicester City v Wolves
10 Agosti 2019 Watford v Brighton
10 Agosti 2019 Tottenham v Aston Villa
11 Agosti 2019 Newcastle United v Arsenal
11 Agosti 2019 Manchester United v Chelsea