picha hii haihusiani na stori.
Akwa Ibom ni jimbo lililo katika ukanda wa kijiografia Kusini mwa nchi ya Nigeria yenye matukio mengi ya ndoa za utotoni.Esther Akan ni miongoni mwa wasichana ambao ni wahaga wa ndoa za utotoni ambapo alipata ujauzito aliopewa na mwanafunzi mwenzake Ernest 30 shuleni akiwa na umri wa miaka 16,ni mtoto wa kwanza kati ya watoto watano, alifiwa na baba yake akiwa na umri wa miaka 12.
Esther
alikuwa mwanafunzi wa SS2 katika Shule ya Sarufi ya Jumuiya ya Sekondari, Ikot
Essien, Ibesikpo-Asutan kaatika Jimbo la Akwa Ibom nchini humo.
Baada
ya hapo Esther alichukua umamuzi wa kuacha shule na kwenda kuishi na aliyempa
ujauzito kama mke na mume , uamuzi ambao anasema sasa anajutia.
Baadae
Esther alifanikiwa kujifungua mtoto wake wa kike, mnamo Januari 2021 mumewe
aliaga dunia muda mfupi baada ya kuthibitisha kuwa Esther alikuwa anatarajia
mtoto wao mwingine wa pili.
"Nilijuta
kuchukua uamuzi huo (ndoa ya mapema). Badala ya kupata, sasa ninateseka zaidi
kuliko hapo awali," Esther aliambia Premium Times.
Angelina
(jina halisi limehifadhiwa), 17, mama mwingine mdogo kutoka kijiji cha Ikot
Obio Ndoho katika eneo la Serikali ya Mtaa ya Mkpat Enin, pia aliacha shule.
Kama Esther, yeye pia alisema amenyanyaswa sana na mwanamume wake.
"Mume
wangu huwa ananinyanyasa; mara nyingi anatumia kuni au mbao kunipiga kila mara
aliniambia kuwa baba yake alimpiga mama yake hadi kumuua, kwa hiyo, anaweza pia
kunipiga hadi kuniua na hakuna mtu atakayefanya chochote," Angelina
alisema.
Alisema
kuwa alipanga baadae kurudi shuleni lakini alishidwa kutokana na mume wake
kumwekea vikwazo vikali.
“Nilipanga
kurejea shuleni pale mambo yatakapokuwa mazuri katika familia yangu, lakini
mume wangu alipokutana nami sikuweza kumpinga kwa sababu nilihitaji msaada na
kwa sababu ya ndoa ya utotoni sikuweza tena kurudi shuleni” Bi Enobong
aliongeza
Serikali ya Akwa Ibom inasema imeendesha
kampeni vikali dhidi ya ndoa za utotoni na matokeo yamekuwa yakipatikana. Mnamo
2020, serikali ilitunga sheria ya kupiga marufuku ndoa chini ya umri wa miaka
16.
Kwa
maneno mengine, wakati serikali ya Nigeria kupitia Sheria ya Haki za Mtoto
inatambua 18 kama umri wa mtu mzima, ni miaka 16 huko Akwa Ibom.
"Tuna
Sheria yetu ya Haki za Mtoto katika Jimbo la Akwa Ibom na umri uliowekwa ni
miaka 16," Naibu Mkurugenzi katika Wizara ya Sheria ya Jimbo la Akwa Ibom
ambaye pia ni Mkurugenzi katika Kitengo cha Kukabiliana na Unyanyasaji wa
Kijinsia na Jinsia, Akwa Ibom. Jimbo, Emem Ette, aliiambia Premium Times.
Alisema
serikali inapinga ndoa za utotoni, kwa hivyo vitendo hivyo ni kosa katika Jimbo
la Akwa Ibom.
"Katika
Jimbo la Akwa Ibom, ikiwa mtoto aliye chini ya umri wa miaka 16 amebakwa au
kupachikwa mimba na mwanamume, iwe ametaka kwa ridhaa yake au la, kwa mujibu wa
sheria, mtu ambaye ni chini ya umri wa miaka 16 hawezi kutoa ridhaa. hivyo
yeyote aliyempa ujauzitoaripoti polisi na kufunguliwa mashtaka kwa kumbaka
mtoto huyo,” alisema.
Alisema
serikali inapinga tabia ya wazazi kukabidhi watoto wao waliopachikwa ujauzito
waolewe na waliopewa ujauzito huo.
“Hakuna
mzazi anayepaswa kumbeba mtoto wao na kusema kwa sababu umempa mimba mtoto
wangu uolewe na mtoto wangu si sawa, sheria ipo kinyume na hiyo ni ukatili
dhidi ya mtu, sheria iko wazi kabisa kuhusu ndoa za utotoni. jimboni," Bi
Ette alisema.
Alisema
juhudi za serikali zilikuwa na matunda, na kulikuwa na kesi chache za ndoa za
utotoni. Kile ambacho serikali inajali zaidi sasa ni kushughulikia mimba za
utotoni, alisema.
Kulingana
na Utafiti wa Demografia na Afya wa Nigeria, 2018, kiwango cha mimba cha kijana
(miaka 15-19) katika Jimbo la Akwa Ibom kilikadiriwa kuwa asilimia 12.8.
Ilikuwa ya tatu kwa juu katika eneo la Kusini-Kusini baada ya asilimia 19.9 ya
Bayelsa na 14 ya Cross Rive
Katika
juudi ya kutatua tatizo hilo Bi Emmanuel mnamo 2015 alizindua Mpango wa
Uwezeshaji wa Familia na Uelekezi wa Vijana (FEYReP) ili kushughulikia tatizo
la mimba za utotoni.
"Mojawapo
ya mwelekeo mkuu wa FEYReP itakuwa jinsi ya kuzuia mimba za utotoni. Baadhi ya
wasichana hawa ni waathirika wa ubakaji na aina nyingine za ukatili wa
kijinsia, kulingana na ripoti ya jinsia nchini Nigeria ya 2012, msichana mmoja
kati ya watatu wenye umri wa miaka 15 hadi 24 wanakabiliwa na unyanyasaji
huu," Bi Emmanuel alisema wakati wa uzinduzi wa programu, kama
ilivyoripotiwa na gazeti la Vanguard.
Kikundi hicho kinatetea uzuiaji wa mimba za
utotoni na kukuza elimu ya mtoto wa kike.
Kamishna
wa Jimbo la Masuala ya Wanawake na Ustawi wa Jamii, Ini Adiakpan, alikiri kwamba
mimba za utotoni bado ni tatizo katika jimbo hilo.
"Katika
Akwa Ibom, tunamlindaje mtoto wa kike? Serikali imeweka utaratibu wa kisheria
kumlinda mtoto; tunayo Sheria ya Haki ya Mtoto, sera ya jinsia na mengineyo.
Pia tunayo elimu bure na ya lazima, ambayo inahusisha watoto wa kiume na wa
kike na kwa wakati huo, kila mtoto anatarajiwa kuwa shuleni," aliiambia
Premium Times.
Katika Akwa Ibom, umri wa utu uzima ni
miaka 16 Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) linakadiria
kuwa asilimia 43 ya wanawake nchini
Nigeria
wenye umri wa kati ya miaka 20 na 24 walifunga ndoa kabla ya kutimiza miaka 18
ambapo takriban asilimia 17 walifunga ndoa kufikia umri wa miaka 15.
Pia,
asilimia 80 ya waliooa kabla ya miaka 18 waliacha elimu sawa na asilimia 39 ya
waliooa kabla ya miaka15.
"Wengi
wao hupachikwa mimba katika hatua za awali, wengine wakiwa na umri wa miaka 14
na wengine wakiwa na miaka 15 au chini zaidi, mara tu jambo hilo likitokea,
watahamia kukaa na mwanamume anayehusika na ujauzito huo." alisema Michael
Udoaba, mkunga wa jadi na kiongozi wa jamii katika jamii ya Okop Ndua Erong.
Wakati
ndoa za utotoni zimekithiri jimbo la Jigawa ambapo ni mojawapo ya majimbo
36 ya Nigeria, yaliyoko katika eneo la kaskazini mwa nchi hali ni mbaya zaidi
huku asilimia 90 ya wasichana chini ya 18 wakiolewa, hali hiyo pia ipo kusini
mwa Nigeria - ingawa katika kiwango cha chini.
kulingana
na repoti ya UNICEF majimbo manne yenye matukio mengi ya ndoa za utotoni kusini
ni Ogun, Oyo, Delta na Akwa Ibom, yenye asilimia 29, 23, 23 na 22.
Mnamo
2018, Akwa Ibom ilikuwa na idadi ya juu ya watoto ambao waliacha shule ya pili
ni Kano ambapo Ibom ililirekodi watoto 581,800 ambao hawakuwa shuleni
huku Kano ikiwa na 989,234, kulingana na Tume ya Elimu ya Msingi kwa Wote,
UBEC.
Akwa
Ibom ilikuwa na idadi kubwa zaidi ya watoto wa kike wasiokwenda shule nchini
ikiwa na 298,161,huku mshindani wake ni jimbo la Sokoto, ilirekodi 270,586.