FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

IJUE FAIDA YA KUNYWA CHAI YA TANGAWIZI NA TANGAWIZI YENYEWE KIAFYA

                                                                           

Na kalebo mussa, Dar Es Salaam
Tangawizi ni mmea kati ya mimea mingi yenye maajabu ,mmea huu unaweza kutumika kama dawa na kutibu magonjwa mengi tu zaidi ya 72 yaliyo ndani ya miili yetu na kutuacha tukiwa wazima na kutekeleza majukumu yetu ya kila siku
Mmea huu unaweza kuonekanika kama mmea wa kawaida na watu kutumia kama mazoea lakini kiungo hiki kinaweza kutumiwa kama dawa , kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au  kikavu kimekaushwa na kutengenezwa unga,
Vilevile tangawizi  maranyingi hutumika  katika nyanja mbalimbali , kiungo katika mboga, dawa ya kutibu  kikohozi, na matumizi mengine vilevile unashauriwa ili kuwa na afya bora kila wakati  tumia chai ya tangawizi kwa wingi ili uweze kujikinga na kutibu magojwa mabalimbali.
a zakeFaida
Huondoa harufu mbaya ya kinywa,
Tofauti na vyakula vingine kama kitunguu swaumu, tangawizi husaidia uwe na harufu nzuri pale unapopumua na kufanya maeneo ya kinywa chako kuwa safi
Tangawizi husaidia msukumo wa damu kuwa mzuri,
Tangawizi husaidia msukumo wa damu mwili kuwa vivzuri hii ni kwa sababu huupa mwili joto la kutosha pindi unapokunywa chai ya tangawizi ambapo mwili huhitaji wakati wa usukumaji wa damu mwilini
Huondoa magonjwa ya asubuhi,
Tanagawizi licha ya kuwa ni tiba ya magonjwa kama kikohozi na mafuta mwilini, tangawizi pia husaidia kupunguza magonjwa ya asubuhi kama uchovu na mninginio, kwa akina mama hasa wajawazito tangawizi huwapunguzia homa za asubuhi pindi wanapoamka , pia hutumika kama kichocheo cha utulivu.
Tangawizi husaidia mfumo wa chakula mwilini
Tangawizi husaidia mwili kunyonya virutubisho kwenye chakula hii husaidiana sana pale unapoamua kupunguza uzito wa mwili na kupata virutubisho vilivyo muhimu tu.
Tangawizi hurekebisha sukari ya mwlii
Husaidia katika kuweka sawa kiwango cha sukari kwenye damu, hapa wagonjwa wa kisukari wanashauriwa kutumia tangawizi  badala ya chai,
Tangawizi huongeza hamu ya kula
Huongeza hamu ya kula chakula kwa wale wenye mfumo mbaya wa umeng’enyaji wa chakula wanashauriwa kutumia tangawizi ili kupata mfumo mzuri wa mmeng’enyo wa chakula
Tangawizi husaidia kuyeyusha mafuta mwilini
Tangawizi husaidia kupunguza kuganda kwa mafuta mwilini ambayo yana madhara makubwa mwilini hasa magonjwa ya kiharusi na shinikizo la damu
Tangawizi husaidia kuondoa sumu mwilini
Tangawizi husaidia kuondoa kichefuchefu na kutapika pia huwasaidi sana wale watu waliotumia sana madawa na kuwa sumu nyingi mwilini
Tangawuzi husaidia kutibu vidonda vya tumbo
Tangawizi pia husaidia mtu mwenye vidonda vya tumbo kwa kupunguza maumivu na hata kuponya vidonda hivyo kama vitakuwa katika hatua ya awali.
Tanagawizi ina kiinilishe muhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu (gingerol) vilevile hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu kwa kitaalamu (constipation related cancer)
Huzuia kuzalishwa kwa bacteria  aitwaye (helicobacter pylori) bacteria huyu ndiye anayesababisha vidonda vya tumbo mwilini pia hutibu kiungulia na kaza mbali mbali za tumbo pia husaidia katika kutibu kansa ya titi,
Pia tangawizi husaidia kutibu kansa za kwenye kizazi na kansa za kwenye mirija ya uzazi, husaidia kuzuia shambulio la moyo, huzuia damu kuganda, hushusha kiwango cha kolesto,husafisha damu , husaidia watu wenye kukamaa mishipa , hutibu maumivu ya tumbo hasa wakati wa hedhi, huimarisha afya ya figo
Ina madini ya manganese ambayo ni muhimu kuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita . tangawizi inakitu kiitwacho (silicon) ambacho cheyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele,meno na kucha pia husaidia umengenyaji wa madini ya calcium
Tangawizi ina vitamin A, C, E, B complex, chuma,zinki, magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta carotene.   
Unaweza kujitibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia zao hili la tangawizi kwa kufuata maelekezo yafuatayo
Kwa wale wenye kuumwa jino na maumivu ya kichwa, unashauriwa kuchukua tangawizi ya unga koroga na maji kidogo iwe nzito kama tope kisha jipake na uchue kwenye paji lako la uso  kabla ya kulala, kwa jino jipake na uchue kwenye shavu
Kwa wenye  maumivu makali ya tumbo unashauriwa kuwa changanya kijiko kimoja au viwili vya tangawizi iliyosangwa na kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya kastoroli kisha kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku
Kujitibu tatizo la kuvimbiwa nakukosa hamu ya kula, unashauriwa kuchangaya juice ya tangawizi , juice ya limao na chumvi mawe kwa vipimo vilivyo sawa hakikisha umechanganya vizuri kunywa dawa hiyo kabla ya kula chakula au changanya vipimo vilivyo sawa sawa vya juice ya tangawizi na sukari ya mawe , koroga vizuri kunywa kabala ya kula chakula. Dawa hii husafisha ulumi na koo na hukuongezea hamu ya kula na kukufanya mchangamfu.
Kujitibu maumivu ya kukoo na kukauka sauti unashauriwa  kutafuana vipande vidogo vya tangawizi vilevile kujitibu tatizo la kuharisha  unashauriwa kuchua sehemu zinazozunguka kitovu kwa juice ya tangawizi
Kwa wale wanaosumbuliwa na kichefuchefu na kutapika kunywa mchanganyiko wa juice ya tangawizi na juice ya kituguu.
Ukiwa na maumivu ya kichwa cha wasiwasi , unashauriwa kuchanganya  juice ya tangawizi na maziwa, kisha kausha  nusa unga huo kama tumbaku.
Maumivu makali ya tumbo, changanya kijiko kimoja cha au viwili vya tangawizi iliyosagwa na kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya kastoroli kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku
Kwa wale wanaojisikia baridi bisi sugu unashauriwa kuchanganya kijiko kimoja cha tangawizi ya unga na vijiko 24 vya maji kunywa mchanganyiko huo ukiwa vuguvugu ,ulale na ujifunike mpaka utoe jasho.
Mmea huu unafanan sana na binzali ikiwa bado haijamenywa maganda yake na kwa hapa Tanzania tangawizi hulimwa sana katika mikoa ya nyanda za juu kusini na baadhi ya mikoa ya kama Kilimanjaro, manayara, morogoro na kwingineko nchini.