ETO’O APINGA VIKALI MADAI YA KUTUMIA UCHAWI KWENYE SOKA LA CAMEROON
Rais wa chama cha soka cha Cameroon, Samuel Eto’o amekanusha madai ya wachezaji
kutumia uchawi katika timu ya taifa nchini huo.
Madai hayo yaliyotolewa katika ripotiya Oktoba 6 na kituo cha Radio France Internation kuwa wanasoka wengi waCameroon wanatumia waganga wa kienyeji. Eto’o amekanusha madai hayo kwa kusema
kuwa matamshi hayo ni dharau kwa wanasoka wote wa Cameroon ambao wameshinda
mashindano na mataji kutokana na juhudi zao.
"Nakanusha rasmi maudhui ya makala
hii na kutoa changamoto kwa waandishi wa wahariri wako kuthibitisha madai yao,"
Eto'o alisema.
Aidha, alisema kuwa ripoti kama hizo haziendani na chombo maarufu
cha habari na kwamba zilikuwa za dharau na zisizofurahisha anaamini katika uhuru
wa kujieleza lakini haamini katika makala za kashfa.