Luka Modric
Kama inavyofahamika Luke Modric ambaye anacheza
katika klabu ya Real Madrid ameongeza kadarasa ya kuendelea kusalia hapo mara
baada ya klabu hiyo kumpa mkataba mpya.
Kutokana na ripoti iliyolipotiwa na AS ilisema kuwa
Modric amekubali kuongeza muda wake wa kukaa hadi 2023, huku kukiwa na chaguo
la miezi 12 zaidi iwapo ataendelea kufanya vizuri.
Modric iwapo atasalia Real Madrid hadi 2024, atakuwa
chini ya miezi mitatu kabla ya kutimiza miaka 39, ingawa hapo awali alitaja
uwezekano wa kucheza hadi atakapofikisha miaka 40.
Modric amefurahia maisha mazuri tangu alipohamia
Uhispania, akishinda Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia la Vilabu mara nne
mfululizo.
Pia ametwaa mataji
mawili ya LaLiga, na vijana wa Carlo Ancelotti watatwaa ubingwa mwingine iwapo
watapata pointi kutoka kwa mechi yao ya nyumbani dhidi ya Espanyol Jumamosi.
Mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 36 amemulika katika michuano ya kimataifa pia, akiwa
nahodha wa Croatia hadi fainali ya Kombe la Dunia mwaka wa 2018.
Aidha, Modri bado hajaonyesha dalili zozote za
kupunguza kasi yake, na kutoa pasi nzuri ya mabao na kuisaidia Real Madrid
katika mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Chelsea.
Hata hivyo, miamba
hao wa Uhispania walijikuta wakiwa nyuma kwa mabao 4-3 baada ya mechi ya kwanza
ya nusu fainali dhidi ya Manchester City, lakini Modric anatumai kurekebisha
kasoro hii kwenye mechi ya marudiano kwenye Uwanja wa Bernabeu siku ya Jumatano
akienda kutafuta Mabingwa wake wa tano.