FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

BECHI LA UFUNDI SIMBA YAKALIA KUTI KAVU


                                        kocha wa Simba Pablo Franco Martin.



 Na kalebo Mussa.


Toka msimu uanze wa ligi kuu ya NBC  Premier  League  Simba Sport Club ambayo imebeba ubigwa kwa takribani misimu minne mfululizo, hali ni tete kutokana na mwenendo wake wa uchezaji na upatikaji matoke.

Timu hiyo ambayo mpaka sasa imecheza mechi 13 katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu imefunga magoli 8, imepoteza mechi 6 ambapo mechi 4 imetoka suluhu na 2 imefungwa.

Benchi la ufundi mpaka sasa limekaa kimya juu ya mwenendo huu wa Simba kitu ambacho kinaleta maswali mengi kwa mashabiki na wadau mbalimbali wa michezo.

Kocha Pablo Franco Martini  akiwa na msaidizi wake Selemani Matola wanaonesha kuishiwa mbinu madhubuti ya kufunia nyavu za magoli, licha ya wachezaji kupiga mashuti ya kulenga goli vilevile kufika mara nyingi katika lango la goli na kushindwa kuweka mpira kimyani mwa maadui zao.

Mitazamo ya mashabiki na wadau wa michezo mbalimbali imekuwa mingi huku wengi wakilalamikia benchi la ufundi kwa kushindwa kufanya kazi yake inayopaswa kama ilivyokuwa katika msimu uliopita ambao Simba ilikuwa na mafanikio makubwa katika mpira.

Idd ki Pazi ‘Father’, kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania ambaye pia aliwahi kuwa goli kipa wa Simba kwenye miaka ya 1990 alisema Yanga na Simba huwa wanapokezana kwahiyo haya ambayo yanatokea kwa Simba ni ya kawaida ispokuwa uongozi unatakiwa usimame imara kuipigania Simba.

“Ungozi  usimame imara kuipigania Simba, mara nyingi mambo haya yakitokea kuna kuwa na mvutano na migogoro sasa sijajua ndani ya Simba yenyewe kuna nini  labda tuone kama ni vitu vya kawaida au ndiyo haya nayoyaona ya zamani, zamani kulikuwa kunanza migogoro ya ndani kwa viongozi wenyewe” alisema Pazi.

Alisema licha ya Simba kuwa na kikosi kipana chenye wachezaji imara bado inashindwa kupata matokeo, kwa kawaida Simba ilikuwa ikienda muda wa mapumziko ikiwa tayari imeshinda magoli kadhaa.

Aidha, Pazi alisema washambualiji wa kimataifa kama , John Bocco amekuwa akikosa magoli ya wazi jambo ambalo siyo la kwaida kulingana na kiwango chake cha uchezaji mpira.

Pazi aliongeza kuwa kocha wa Simba Pablo bado anaonekana kuvurugika katika mbinu zake za kupanga kikosi na cha kuleta ushindi  labda huenda amekuja katika msimu mbaya.  

“Simba bado haijasimama kwa mfano majirani zetu wakipanga timu inapagika lakini sasa hivi kwa upande wa simba bado timu inamvuruga Palo” alisema.