FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

SAMAKIBA FOUNDATION WATAMBIANA KIBABE


Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ali Salehe ‘Alikiba’ amefunguka kuwa Team Kiba hawatakubali tena kufungwa na Team Samatta katika mechi ya hisani ya SamaKiba Foundation ambao unakwenda kupigwa Uwanja wa Taifa Dar, Agosti 8, mwaka huu.

King Kiba amesema walikuwa na bahati mbaya katika misimu miwili iliyopita na kujikuta wakifungwa katika mechi zote mbili, licha ya kuwa kikosi chao kilikuwa bora zaidi ya kile cha Team Samatta, hivyo awamu hii ni ni zamu yao kuwapa raha mashabiki wa TeamKiba.

Mchezo huo wa SamaKiba Foundation ulianzishwa kwa kuunganisha nguvu kati ya nahodha wa Taifa Stars na nyota wa Aston Villa ya England, Mbwana Samatta na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba kwa lengo la kukusanya fedha na kuzisaidia jamii za watu wa hali ya chini.

Mbwana Samatta tayari ameshatangaza timu ya watu watano ambao ni Mohamed Samatta, Idd Seleman ‘Nado’, Farid Mussa na Juma Kaseja na msemaji wake ni Haji Manara, ambaye ni Ofi sa Habari wa klabu ya Simba.

Huku wasanii wake wawili wa Kings Music, K2ga na mdogo wake Abdu Kiba wakitajwa kuwa sehemu ya kikosi hicho.

Matokeo yaliyopita yalikuwa hivi, msimu wa kwanza ambao ulikuwa ni Juni Mosi, 2018, Team Samatta 3-1 TeamKiba, huku msimu wa pili uliofanyika Juni 11 mwaka jana, Team Kiba walifungwa 6-3.

Hivyo sasa wapenzi wa michezo wawe tayali kupata burudani ya kipekee katika siku hiyo maalumu.


ZUCHU AMKUNA LADY JAYDEE

Msanii wa Bongo Fleva, Judithi Wambura ‘Lady Jaydee’ amesema kuwa msanii mpya wa Lebo ya Wasafi Classic, Zuchu atafika mbali kutokana na juhudi zake.

Lady Jaydee amesema kuwa Zuchu amekuwa na juhudi ya kutaka kukutana na watu waliotangulia ili kujifunza na hicho ndicho kitamfikisha mbali.

“Zuchu ana juhudi za kuwa karibu na watu waliomtangulia kwenye gemu, hii itamfanya kufika mbali zaidi na anajitahidi hata kwenye kazi zake.

Pia amesema kuwa kama sisi zamani tulikuwa tunawaongelea wanamuziki kama mama yake mzazi (Malkia Khadija Kopa), hiyo ni nzuri sana,’’. alisema Lady Jaydee.


TAKEOFF AKABILIWA NA TUHUMA NZITO

Mwanamke mmoja huko Jijini Los Angels nchini Marekani amemshitaki Rapa anaeunda kundi la Migos , Kirshnik Khari Ball ‘Takeoff’ kuwa alimbaka walipokua kwenye Party mjini humo huku akisisitiza kuwa ana ushahidi kutoka Hospitali .

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ , mwanamke huyo amesema kuwa Takeoff alimlazimisha kuwa karibu nae Chumba cha mtu aliyemualika katika Party hiyo .