FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

BASATA YATOA RUKSA SHERIA IZINGATIWE



Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), wametoa shukrani za dhati kwa Rais Magufuli kwa kurejesha shughuli za kisanaa kama ilivyokuwa awali, baada ya kuzuiliwa kwa muda kutokana na janga la Corona.

Godfrey Mngereza alisema kuwa, walikuwa wamekaa vikao na wadau wote wa sanaa ili kujadili jinsi gani watafanya shughuli hizo licha ya uwepo wa ugonjwa wa Corona.

"Tayari tulikuwa tumekaa vikao na wadau wote wa sanaa siku ya Mei 28 ili kuangalia ni namna gani ambavyo tunaweza kufanya kazi zetu huku tunaishi na Corona,
tulichukua yale maoni na tukapeleka Wizarani, ndiyo maana Rais mwenyewe alitoa tamko ili kurejesha shughuli za michezo, sanaa na burudani, na sisi kama BASATA tumetoa ruksa, lakini haina maana wasanii wavunje sheria na kanuni" Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza.

Ikumbukwe kwamba hii imekuja mara baada ya Rais Magufuli kutoa tamko la kuruhusu shughuli zote ziendelee kama kawaida wakati alipokuwa anavunja Bunge la 11 jijini Dodoma june 16.  






YOUNG DEE AFUNGUKA KUHUSU DAWA ZA KULEVYA


Msanii wa Bongo Fleva, David Ganzi ‘Young Dee’ amefunguka namna ambavyo alipitia wakati mgumu wa kutumia dawa za kulevya.

Akiweka wazi jambo hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram Young Dee aliandika kuwa haikuwa rahisi kwa yeye kuondokana na tatizo hilo kwani madaktari walifanya kazi ya ziada sana.

“Kuna muda nikikumbuka baadhi ya mapito yangu huwa naishia kucheka tu (Swipe Left ucheke). Mwaka 2016 nilipambana sana kuachana na hili swala, kwa msaada wa watu wengi. Haikuwa rahisi washkaji zangu, ila Mungu yu nami na alinipigania sana.

Kuna sababu kadhaa zilizopelekea kunisaidia kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya (Hivi karibuni Documentary yangu ikitoka, mtajua namna nilivyoingia kwenye hilo swala). Sababu ya kwanza ilikuwa ni team yangu ya kipindi kile ya MDB. Kusema ukweli hawa watu walipambana sana na jambo langu, nadhani sikupigwa makofi tu ila niliwakwaza sana. Walipambana sana kunitoa huko.

Japo haikuwa rahisi hata kidogo, Sababu ya Pili ni Mh. Baba Keagan na kampeni ya kuzuia madawa. Ile ilikuwa na matokeo chanya sana kwa jamii hasa kwangu mimi. Najua Mh. Makonda alipigwa vita sana kwenye swala lile, na najua wapo ambao hadi leo wanaliona jambo lile lilikaa kisiasa, lakini mimi nina ushuhuda wa namna kampeni ile ilivyonisaidia mimi binafsi, na baadhi ya vijana ninaowafahamu, ambao leo hii tunaendesha maisha yetu na familia zetu baada ya kulazimika kuacha kabisa 

matumizi ya madawa ya kulevya kutokana na shinikizo la serikali.
Wazee, msichokijua ni kwamba kuna siku nilizidisha dozi, nikajiona kabisa nakufa. Siku hiyo nilisali sala mbili, ya kwanza ni ya mwisho, na ya pili ilikuwa ya kumuomba Mungu anivushe ule usiku tu, nami nilimuahidi kuto kurudia tena na shughuli hizo. (Story nyingi mtazipata kwenye Documentary yangu); Baba Keagan kwa namna moja au nyingine najua ulikutana na changamoto kubwa sana wakati wa kampeni ile, 

kwasababu ulipigana vita kubwa sana.
Mimi na familia yangu tuchukue fursa hii kwanza kukupa pole kwa kadhia zote ulizokutana nazo, na pia naomba niseme asante sana kwa kuileta. Imenisaidia sana, huenda leo hii ningekuwa teja kabisa nisiye na thamani machoni mwa watu, lakini kwa nguvu za Mungu, leo naweza kuandika hapa na kushare a positive note kutoka kwenye janga negative kwenye maisha yetu vijana” aliandika Young Dee.
Chidi Benzi, Ray C na wengine ni moja ya mastaa ambao walipitia changamoto ya dawa za kulevya.





HARMONIZE ATIMIZA AHADI YAKE KWA 
LADY JAY DEE


 Msanii wa  Bongo Flave, Abdul Rajabu ‘Harmonize’ baada ya kuitoa hivi karibuni na single aliyoshirikishwa na mwanadada Nandy, mara hii anakuja na  toleo jipya akiwa na msanii mkongwe Lady Jaydee.


Nyimbo hiyo ambayo inaitwa ‘wife’ video yake imeachiwa juzi mashabiki wameifurahia kuwa kali pamoja na mazingira yake ni mazuri.

jana Harmonize ameuposti wimbo huo katika ukurasa wake wa ‘Twitter’ huku akielezea jinsi alivyokuwa na ndoto ya muda mrefu ya kuimba na Lady Jaydee.

“Ilikuwa ndoto yangu ya siku nyingi kufanya kazi na dada yangu kipenzi Jidejaydee trust me i'm big fan of her! nimeanza kumsikia na kumuona tangu nikiwa mtoto finally dream come true brand new clapper boardclapper board wife elephant ft Jidejaydee” aliandika Lady Jaydee.