FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

PIERRE AELEZA ALIVYOPONA CORONA “NAMUAMINI MUNGU TU”




Msanii wa vichekesho nchini, Peter Mollel  ‘Pierre Liquid’ ameeleza namna ambavyo alivyopona ungonjwa wa Covid 19,awataka Watanzania kutokuwa na hofu dhidi ya ungonjwa huu

Akizungumza kwa nyakati tofauti Pierre alisema kuwa kwa kiasi kikubwa mazoezi yalimsaidia kupata unafuu kwa uharaka sana.

“Niliwekwa karantini Amana nikawa natumia dawa nikawa nameza pia kingine nikawa nafanya mazoezi ya viungo, kwakeli yamenisaidia sana kwasababu nilikuwa siwezi kupumua vizuri lakini baada ya kuwa nafanya yale mazoezi niakajikuta mapafu yanapanuka vizuri.

 kwahiyo kuanzia hapo nikawa natoa pumuzi vizuri tofauti na mwanzo nikasema basi kumbe mazoezi yanasaidia toka hapo maumivu ya kichwa nayo yakawa yameondoka kifua tena kikawa hakiumi tena mbavu zilikuwa zinanibana sana nazo zimeacha kubana mpaka sasa hivi niko vizuri namshukuru Mungu.
Mungu atusaidie kabisa na atuepushie na huyu mdudu ambaye anatusakama katika nchi yetu.” Alisema  Pierre

Aidha aliongeza kwa kuwataka Watanzania wasiwe na hofu bali wawe na ujasiri wa kwenda kupima endapo wanapokuwa wamejihisi kuwa na dalili zinazofanana na ungonjwa huo.

“Nachosema kwamba kwa Watanzania wenzangu wasihofu kwenda Hospitalini  wanapopata zile dalili waende mara moja kwasababu unapoenda kule mapema ndipo unapoweza kupata nafuu vizuri kama mimi nilivyoweza kupata nafuu haraka sana kwababu  nilipogundulika na huo ungonjwa nikaenda na kama hivi nimetoka, inamaana inawezekana ukapona kama nilivyo vizuri . nilikuwa nakula machungwa,maji ya limao,tangawizi ni hivo tu basi” aliongeza.


Beyonce kuunga mkono sekta ya afya


Msanii kutoka nchini Marekani, Beyoncé Giselle Knowles ‘Beyonce’ akiwa na mama yake mzazi, Bi. Tina Knowles wameamua kuchangia Sekta ya Afya kwa kujitolea vifaa vya kupima virusi vya Corona pamoja na vifaa vingine muhimu kwa watu kujikinga.

Beyonce na Mama yake kupitia tovuti yake ameanzisha kampeni iitwayo ‘IDidMyPart’ ambayo inawahamasisha jamii ya watu weusi kuweka kipaumbele suala la afya zao kwenye janga hili la Corona.

Aidha lengo la kampeni yao ni kwa watu maarufu kuchangia kupitia tovuti hiyo , mpaka sasa Tyler Perry tayari  ameonesha nia ya   kutoa vifaa vya upimaji wa Corona mjini Atlanta Georgia.
Ikumbukwe kwamba kabla ya kuja na kampeni hii Beyonce ameshawahi kuchangia  kiasi cha ($6 million) sawa na Bilioni 13.8 za Kitanzania kwa asasi za huduma za kijamii kwa ajili ya kuchangia vifaa tiba mjini New York, Houston, Detroit.


Wema alamba dili nono

Msanii wa Bongo Movie ambaye pia kwa sasa amejikita kwenye mapishi kupitia kipindi chake cha ‘CookwithWemaSepetu’ ,Wemu Abrahamu ametangazwa rasmi kuwa balozi wa sosi ya nyanya (Tomato Sauce) kutoka kampuni ya RedGold.

Akiongea na Waandishi wa Habari jana Wema alibainisha kuwa RedGold ni bidhaa zinazotengenezwa na Darsh Industries Tanzania  ambapo wana bidhaa nyingine nyingi zikiwemo Tomato Sauce, Chilli Sauce, Jams, Juice na Ketchup.

 Aidha aliongeza kuwa Kampuni hiyo ya RedGold ndio wadhamini wa kwanza kwenye kipindi chake cha Mapishi kinachoruka kupitia kwenye Application yake iitwayo WemaApp.

Hata hivyo kupitia ukurasa wake wa Instagram alionesha furaha yake namna ambavyo anafurahia kuwa mwanafamilia wa RedGold.
“Ninayo furaha kutangaza Rasmi kuwa Mimi ni Brand Ambassador wa RedGold na pia RedGold ndo Sponsor wetu wa kwanza kabisa kwenye kipindi chetu pendwa cha Cook with Wema Sepetu kinachoruka kupitia Application yangu... .”aliandika Wema.