FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

OMMY DIMPOZ AWEKA WAZI SUALA LA KUOA


Msanii wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ ameweka wazi suala la kuoa na kwa sasa yupo kwenye maandalizi na panapo maajaliwa ataweza kufunga ndoa hivi Karibuni.

Ommy ameweka wazi jambo hilo alipokuwa mbashara katika ukurasa wake wa Instagram ambapo alisema kuwa kwasasa ameanza maandalizi madogo madogo ikiwemo kufuga ndevu ili hata akienda kuposa aonekane ni kijana anaejielewa.

Aidha aliongeza kuwa alitaka kuoa kipindi hiki cha Ramadhan lakini akaogopa asije kuuziwa mbuzi kwenye gunia.



 HARMONIZE AZUA NGUMZO KUBWA MTANDAONI 


Msanii wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ amezua gumzo kubwa, ampigia simu Jacqueline Wolper,Sarah amtaka mpenzi wake aende nyumbani kwa Nicole.

Harmonize alipokuwa live na Jacqueline Wolper katika ukurasa wake wa Instagram mashabiki wengi wali-comment kutaka warudiane pia wengine walishangazwa na tukio hilo la Harmonize kuwasiliana na EX wake hadharani.

Gumzo  kubwa lilikuja ambapo,Harmonize alipokuwa live kwenye Instagram akiongea na video vixen, Nicole katika wimbo wake wa  "Bedroom" ambapo mke wake, Sarah aliandika commet kuwa "Baby nenda salimia Nicole nyumbani".

Comment hiyo ililetea sura tofauti kwa Nicole kisha kumwambia, Sarah kuwa yeye hawako kwenye mahusiano ya kimapenzi na Harmonize kama ambavyo imekuwa ikienezwa mtandaoni.
“Wengine wanaongea maneno mabaya, unaona comment, Baby nenda salimia Nicole nyumbani, Why!, why!, why!, Sarah i don’t live with Harmonize in my home,” alisema Nicole kisha na kuondoka katika line.




                    HABARI NJEMA KWA MEEK MILL


Msanii kutoka nchini Marekani, Robert Rihmeek Williams ‘Meek Mill’ na mpenzi wake, Milan Harris wamefanikiwa kupata mtoto wa kiume.

Meek Mill ameweka jambo hilo wazi Mei 6,2020 katika ukurasa wake wa ‘Twitter’  ambapo siku hiyo pia alikuwa anasherehekea  siku yake ya kuzaliwa.

Meek Mill ameiita hii ni zawadi yake bora kabisa kwake na huyu anakuwa mtoto wake wa tatu, tayari ana watoto wawili wa kiume Murad Williams na Rihmeek Williams.




 HAMISA MOBETTO AWATAKA VIJANA JAMBO HILI


Msanii wa Bongo Fleva na mwanamitindo , Hamisa Mobetto jana ametambulishwa rasmi kuwa mwanafamilia wa taasisi ya Smart Generation.

Taasisi hiyo inajikita kuchukua watu ambao wanaushawishi mkubwa katika jamii ili kuweza kuwahamasisha vijana katika nyanja mbalimbali

Mwanamitindo huyo ambaye anaushawishi mkubwa hasa katika mitandao ya kijami aliweka wazi namana ambavyo atajikita kuwashawishi vijana kuwa makini katika suala la uzazi wa mpango
“Tukiwa kwenye taifa lenye uwazi na ukweli ni vizuri kwa kila kijana ambaye ametimiza umri wa kuwa kwenye mahusinao kuchukua hatua ambazo zinafaa wakati wanaanza mahusiano ili kuepuka mimba ambazo hawajatalajia na hii inaenda kwa pande zote mbili kwa maana ya wanaume na wanawake”. alisema Mobetto.

“Tukiwa kama taifa ningependa kushauri kwa kila kijana wakati wakuanza mahusiano ni wakati pia sahihi wakujipanga katika maisha yako usilete kitu chochote kikwaze wewe kutimiza malengo ama ndoto zako katika maisha, vituo vya afya tunavyo vingi nchi nzima ni vizuri kila mtu aende kwenye vituo hivyo akapate ushauri na kuna njia tu za kujizuia kupata ujauzito kama hauko tayari kwa kutumia uzazi wa mpango kuna mipira na njia nyingi”.aliongeza

Aidha C.E.O wa SMART GENERATION, Siza akiwa na Msanii wa Bongo Fleva Nikki Wa Pill  alisema kuwa lengo kubwa ambalo wanalitizamia ni kuwawezesha vijana wa Kitanzania kuweza kutumia vipaji vyao ili kufika mbali.