FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

Wachezaji wa Uingereza kutotumia Wi-Fi kombe la dunia Urusi




Wachezaji wa Uingereza na wafanyikazi wake watashauriwa kutotumia mtandao wa Wi-fi katika maeneo ya uma ama hata katika hoteli wakati wa kombe la dunia la mwaka ujao nchini Urusi kutokana na hofu ya kudukuliwa.
Shirikisho la soka nchini Uingereza lina wasiwasi kwamba habari muhimu kama vile majeraha , kikosi kitakachochaguliwa pamoja na maelezo mengine ya kiufundi huenda zikadukuliwa.
Hofu ya wizi wa data pia imeangaziwa kufuatia udukuzi wa mwezi uliopita uliofanywa na kundi la Fancy Bears kuhusu matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku katika soka.
Kundi hilo linadai kwamba habari hizo zilizofichuliwa mnamo mwezi Agosti zinaonyesha kwamba takriban wachezaji 160 walifeli vipimo vya utumizi wa dawa za kusisimua misuli 2015, huku idadi hiyo ikidaiwa kuongezeka na kufikia 200 mwaka uliofuta.
FIFA inasema inaendelea kuzuia mashambulizi ya kiusalama.