FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

Vodacom kuvunja rekodi ya mauzo ya DSE soko la awali





WAWEKEZAJI zaidi ya 40,000 wamevutiwa na hisa za Vodacom Tanzania PLC zinazoendelea na mchakato wa kuingia sokoni. Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao, alisema hisa hizo zitakuwa za kihistoria na zitavunja rekodi kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam kwa miaka 19 tangu kuanzishwa kwake.

Hii imechangia kwa kiasi kikubwa na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutaka kuona Watanzania wanakuwa wamiliki wa kampuni kubwa zinazofanya biashara nchini.
Biashara katika hisa za Vodacom Tanzania PLC kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam inatarajiwa kuanza mwezi huu baada ya kukamilika kwa taratibu za uhakiki unazofanywa na Mamlaka ya Masoko na Mitaji Tanzania (CMSA).
Katika taarifa yake, Ferrao alisema, “Vodacom Tanzania PLC inajivunia kuwa kampuni ya mawasiliano inayoongoza hapa Tanzania na ndiyo maana leo hii tumekuwa kampuni ya kwanza kutimiza masharti ya Bunge la Tanzania ya kutaka makampuni zote za simu za mkononi kuorodhesha hisa zake kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam.”
Vodacom Tanzania PLC kupitia kwa mshauri wake mkuu, kampuni ya Orbit Securities, imekabidhi kwa Mamlaka ya Masoko na Mitaji Tanzania (CMSA) majina ya wote walionunua hisa hizo kwa ajili ya,” alisema Ferrao