FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

USHINDANI WA KIBURUDANI HUSAIDIA KUONGEZA KASI YA UBUNIFU KATIKA MUZIKI


Burudani ni moja ya kitu ambacho kinampa mtu uchangamfu fulani madharani mtu anapokuwa anasikiliza wimbo ambao anaupenda hujisikia furaha sana kulingana na mshairi ya nyimbo hiyo yalivyomvutia.

Msanii hutumia akiri nyingi sana kukaa na kuwaza namna ambavyo anaweza kutunga wimbo ambao jamii itaipokea kwa mikono miwili pia kuhakikisha kwamba lengo alilolikusudia linakamilika kwa asilimia kubwa.

Mara nyingi msanii anapotunga wimbo na kuuleta kwenye jamii kwanza huangalia mashabiki wake wanahitaji muziki wa aina gani ambao utakuwa rahisi kukonga nyoyo za mashabiki wake na kuzidi kumuamini katika kazi zake pia huwa makini sana katika kazi yake ambayo anaifanya.

Tukija katika suala la mashairi bora kwa kila msanii hapo ndipo ushindani unaanzia wa kiburudani ambapo kila mmoja wapo atahitaji kuona kwamba muziki wake unakuwa mkubwa kwa kumshinda mwingine ili kuwa kinara.

Lakini katika ushindani huo wengi wao nyota zao hushindwa kungara kwa sababu mbalimbali ikiwemo pesa, kukosa uongozi imara (management), support ya mashabiki, ubunifu katika muziki, kukosa soko la kuinua muziki huo kwasababu muziki ni biashara lazima pawepo na sehemu husika ya kuuza bidhaa hizo.

Hivyo ni wasanii wachache sana ambao nyota zao zimengara nakuweza kupanua mbawa zao kitaifa na kimataifa madharani katika muziki wasasa wa Bongo Fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, Ali Salehe ‘King Kiba’ Rajabu Abdul ‘Harmonize’ ni moja ya wasanii ambao nyimbo zao zinapendwa sana kusikilizwa na kuchezwa ukilinganisha na nyingine. Mfano nyimbo kama Sound,Baba lao zote za Diamond, mshumaa ya Ali kiba, Uno ya Harmonize.

Hata hivyo haujasahaulika muziki wa zamani amabao mpaka sasa ukichezwa sehemu unaonekana kama umetoka jana, moja ya wasanii waliokuwa mashuhuri katika muziki Albert Keneth Mangwair ‘Albert Mangwea’ amabaye ni marehemu kwa sasa ambapo alitamba kwa vibao vingi  She got a gwan, mikasi ,Alma, Kimya Kimya akishirikishwa na Jay Moe.
Tukiwa katika msimu maalumu wa kuazimisha miaka 58 ya uhuru wa Tanzania kwa sasa muziki wa Bongo umekuwa na ushindani mkubwa sana ambapo kila kundi linahitaji kuwa kinara kwa kuonekana kuwa na mashabiki wengi sana katika muziki wao.

Madharani katika tamasha hizi zinazoendelea Wasafi Festival, Tigo Fester, Unfogettable Tour, muziki mnene, Nandy Festival ni makundi ambayo yanashindana sana katika uwanja wa kiburudani, ambapo kila mmoja anaona yuko bora kuliko mwingine.

Tukichukua makundi mawili hapo Wasafi Festival na Tigo Fester ni makundi ambayo ni gumzo katika muziki wa Kibongo kwa kuona kila mmoja yuko bora kuliko mwingine katika utoaji burudani pia kuwa na ushawishi wa mashabiki wengi katika matasha hayo.

Hali hii imesababisha makundi haya kutambiana sana kwa kuonekana kuwa na mashabiki wengi pindi wanapofanya maonesho mbalimbali.

Hivi karibuni kulitokea sekeseke katika mitandao ya kijamii kwa makundi haya kuonesha ubabe wa kujaza watu wengi katika matamasha ambayo yalifanyika hivi karibuni.
Hali hii imesababisha kuleta mgawanyiko wa mashabiki katika pande mbili tofauti. Huku ikonekana upande mmoja kuwa na mashabiki wengi kuliko sehemu nyingine.

Hii inaleta maana ngani katika burudani, katika kuchunguza zaidi unaweza kuona kwamba tatizo kubwa lipo kwenye ubunifu wa ndani kwa kuweka vitu vya tofauti ambapo upande mwingine umeshindwa kufanya hivyo. Diamond amekuwa mbunifu sana kusoma mchezo wa kiburudani haraka ambapo mpaka sasa amejiwekea misingi imara ambayo siyo rahisi kuimbomoa.
  
Vilevile mara nyingi amekuwa akitoa nyimbo ambazo zinagusa kundi kubwa la mashabiki hivyo kupeleka kupendwa zaidi.

Media kwa media pia zimekuwa ni moja ya kuleta ushindani wa kiburudani madharani Wasafi Fm na Clouds Fm ni media ambazo  zinaushindani mkubwa wa muziki lakini kwa asilimia kubwa wengi wamekuwa wasikilizaji sana upande mmoja.

Katika hali hii itasababisha kila upande kuzidi kubuni vitu mbalimbali ambavyo hakika vitazidi kumuweka kuwa kinara katika muziki ambao anaufanya lengo ikiwa ni kuweka ushindani zaidi.





Nuh Mziwanda adai kupelekwa kwa mganga na Shilole



 Msanii na mtayarishaji wa muziki, Nuh Mziwanda, amefunguka madai ya kuchukuliwa nyota ya kimuziki na kimaisha, pamoja na suala la kupelekwa kwa mganga na aliyewahi kuwa mpenzi wake Shilole.

Nuh Mziwanda, amewajibu mashabiki ambao wanadai amechukuliwa nyota yake na mpenzi wake huyo wa zamani kwa kusema, hajui kama amechukuliwa nyota yake ila anachojua alikuwa kimya kwa muda mrefu.

"Kama mashabiki wanahukumu hivyo ni sawa ila ukimya wangu nilikuwa bize narekodi, kufanya kazi, mimi naona nipo sawa nafanya mambo yangu kimpango wangu pia siamini katika vitu kama hivyo ila kama watu wanaamini sawa labda wao wanamjua yule bi Dada kama ni mchawi mchawi" alisema Nuh Mziwanda.

Aidha Nuh aliongeza kuwa , aliwahi kupelekwa kwa mganga na Shilole.

"Wakati naachia wimbo wa jike shupa aliniambia niende kwa mganga, ili nijue nyimbo gani kali naiachia baada ya jike shupa pia akamtumia rafiki yangu Beka ili anishawishi kwenda kwa mganga na nilivyokubali tu kesho yake asubuhi alinifata tukaingia kwenye gari akanipeleka kwa mganga Tanga"aliongeza.






Davido ameukosoa mwenendo wa siasa nchini Nigeria



 Staa wa muziki nchini Nigeria, David Adedeji Adeleke ‘Davido’ ameukosoa mwenendo wa siasa nchini Nigeria, akisema taratibu demokrasia imeanza kuota mbawa nchini humo.

Davido aliyasema  hayo apotakiwa kutoa maoni yake juu ya kitendo cha kukamatwa kwa kinara wa vuguvugu la Revolution Now Movement, Omoyele Sowore.

Kupitia ukurasa wake wa ‘Twitter’, Davido aliandika: “jusitice slowly becoming a think of the past our dear country….”.  “Haki imeanza kuwa historia katika nchi yetu pendwa…”.




           



             Miss Universe 2019 ashinda kwa kishindo


 Nchi ya Afrika ya Kusini yaibuka kidedea na kuendeleza historia yake kwa mwaka huu wa 2019 kupitia kwa mlimbwende Zozibini Tunzi (26) baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya Miss Universe yaliyofanyika Atlanta, Georgia Kwenye studio za Tyler Perry.

Zozibini Tunzi amefanikiwa kutwaa Taji hilo ambalo lilikuwa linashikiliwa na Catriona Gray Kutoka Ufilipino.

Mara ya mwisho kwa Afrika Kusini kushinda Taji hili ilikuwa mwaka 1978 na mara ya pili ni mwaka 2017.