Wednesday 12 October 2022

ETO’O APINGA VIKALI MADAI YA KUTUMIA UCHAWI KWENYE SOKA LA CAMEROON

Rais wa chama cha soka cha Cameroon, Samuel Eto’o amekanusha madai ya wachezaji kutumia uchawi katika timu ya taifa nchini huo. Madai hayo yaliyotolewa katika ripotiya Oktoba 6 na kituo cha Radio France Internation kuwa wanasoka wengi waCameroon wanatumia waganga wa kienyeji. Eto’o amekanusha madai hayo kwa kusema kuwa matamshi hayo ni dharau kwa wanasoka wote wa Cameroon ambao wameshinda mashindano na mataji kutokana na juhudi zao. "Nakanusha rasmi maudhui ya makala hii na kutoa changamoto kwa waandishi wa wahariri wako kuthibitisha madai yao," Eto'o alisema. Aidha, alisema kuwa ripoti kama hizo haziendani na chombo maarufu cha habari na kwamba zilikuwa za dharau na zisizofurahisha anaamini katika uhuru wa kujieleza lakini haamini katika makala za kashfa.

No comments:

Post a Comment

nice