Burudani ni moja ya kitu ambacho kinampa mtu
uchangamfu fulani madharani mtu anapokuwa anasikiliza wimbo ambao anaupenda
hujisikia furaha sana kulingana na mshairi ya nyimbo hiyo yalivyomvutia.
Msanii hutumia akiri nyingi sana kukaa na kuwaza
namna ambavyo anaweza kutunga wimbo ambao jamii itaipokea kwa mikono miwili pia
kuhakikisha kwamba lengo alilolikusudia linakamilika kwa asilimia kubwa.
Mara nyingi msanii anapotunga wimbo na kuuleta
kwenye jamii kwanza huangalia mashabiki wake wanahitaji muziki wa aina gani
ambao utakuwa rahisi kukonga nyoyo za mashabiki wake na kuzidi kumuamini katika
kazi zake pia huwa makini sana katika kazi yake ambayo anaifanya.
Tukija katika suala la mashairi bora kwa kila
msanii hapo ndipo ushindani unaanzia wa kiburudani ambapo kila mmoja wapo
atahitaji kuona kwamba muziki wake unakuwa mkubwa kwa kumshinda mwingine ili
kuwa kinara.
Hivyo ni wasanii wachache sana ambao nyota zao
zimengara nakuweza kupanua mbawa zao kitaifa na kimataifa madharani katika
muziki wasasa wa Bongo Fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, Ali
Salehe ‘King Kiba’ Rajabu Abdul ‘Harmonize’ ni moja ya wasanii ambao nyimbo zao
zinapendwa sana kusikilizwa na kuchezwa ukilinganisha na nyingine. Mfano nyimbo
kama Sound,Baba lao zote za Diamond, mshumaa ya Ali kiba, Uno ya Harmonize.
Tukiwa katika msimu maalumu wa kuazimisha miaka
58 ya uhuru wa Tanzania kwa sasa muziki wa Bongo umekuwa na ushindani mkubwa
sana ambapo kila kundi linahitaji kuwa kinara kwa kuonekana kuwa na mashabiki
wengi sana katika muziki wao.
Madharani katika tamasha hizi zinazoendelea
Wasafi Festival, Tigo Fester, Unfogettable Tour, muziki mnene, Nandy
Festival ni makundi ambayo yanashindana sana katika uwanja wa kiburudani, ambapo
kila mmoja anaona yuko bora kuliko mwingine.
Tukichukua makundi mawili hapo Wasafi Festival na
Tigo Fester ni makundi ambayo ni gumzo katika muziki wa Kibongo kwa kuona kila
mmoja yuko bora kuliko mwingine katika utoaji burudani pia kuwa na ushawishi wa
mashabiki wengi katika matasha hayo.
Hali hii imesababisha makundi haya kutambiana
sana kwa kuonekana kuwa na mashabiki wengi pindi wanapofanya maonesho
mbalimbali.
Hivi karibuni kulitokea sekeseke katika mitandao
ya kijamii kwa makundi haya kuonesha ubabe wa kujaza watu wengi katika
matamasha ambayo yalifanyika hivi karibuni.
Hali hii imesababisha kuleta mgawanyiko wa
mashabiki katika pande mbili tofauti. Huku ikonekana upande mmoja kuwa na
mashabiki wengi kuliko sehemu nyingine.
Hii inaleta maana ngani katika burudani, katika
kuchunguza zaidi unaweza kuona kwamba tatizo kubwa lipo kwenye ubunifu wa ndani
kwa kuweka vitu vya tofauti ambapo upande mwingine umeshindwa kufanya hivyo.
Diamond amekuwa mbunifu sana kusoma mchezo wa kiburudani haraka ambapo mpaka
sasa amejiwekea misingi imara ambayo siyo rahisi kuimbomoa.
Vilevile mara nyingi amekuwa akitoa nyimbo ambazo
zinagusa kundi kubwa la mashabiki hivyo kupeleka kupendwa zaidi.
Media kwa media pia zimekuwa ni moja ya kuleta
ushindani wa kiburudani madharani Wasafi Fm na Clouds Fm ni media ambazo zinaushindani mkubwa wa muziki lakini kwa
asilimia kubwa wengi wamekuwa wasikilizaji sana upande mmoja.
Katika hali hii itasababisha kila upande kuzidi
kubuni vitu mbalimbali ambavyo hakika vitazidi kumuweka kuwa kinara katika
muziki ambao anaufanya lengo ikiwa ni kuweka ushindani zaidi.
Nuh Mziwanda adai kupelekwa kwa mganga na Shilole
Nuh Mziwanda, amewajibu mashabiki ambao wanadai
amechukuliwa nyota yake na mpenzi wake huyo wa zamani kwa kusema, hajui kama
amechukuliwa nyota yake ila anachojua alikuwa kimya kwa muda mrefu.
"Kama mashabiki wanahukumu hivyo ni sawa ila
ukimya wangu nilikuwa bize narekodi, kufanya kazi, mimi naona nipo sawa nafanya
mambo yangu kimpango wangu pia siamini katika vitu kama hivyo ila kama watu
wanaamini sawa labda wao wanamjua yule bi Dada kama ni mchawi mchawi" alisema
Nuh Mziwanda.
Aidha Nuh aliongeza kuwa , aliwahi kupelekwa kwa
mganga na Shilole.
"Wakati naachia wimbo wa jike shupa
aliniambia niende kwa mganga, ili nijue nyimbo gani kali naiachia baada ya jike
shupa pia akamtumia rafiki yangu Beka ili anishawishi kwenda kwa mganga na
nilivyokubali tu kesho yake asubuhi alinifata tukaingia kwenye gari akanipeleka
kwa mganga Tanga"aliongeza.
Davido ameukosoa mwenendo wa siasa nchini Nigeria
Staa wa muziki nchini Nigeria, David Adedeji
Adeleke ‘Davido’ ameukosoa mwenendo wa siasa nchini Nigeria, akisema taratibu
demokrasia imeanza kuota mbawa nchini humo.
Davido aliyasema hayo apotakiwa kutoa maoni yake juu ya kitendo
cha kukamatwa kwa kinara wa vuguvugu la Revolution Now Movement, Omoyele
Sowore.
Kupitia ukurasa wake wa ‘Twitter’, Davido
aliandika: “jusitice slowly becoming a think of the past our dear country….”. “Haki imeanza kuwa historia katika nchi yetu
pendwa…”.
Miss Universe 2019 ashinda kwa kishindo
Nchi ya Afrika ya Kusini yaibuka kidedea na
kuendeleza historia yake kwa mwaka huu wa 2019 kupitia kwa mlimbwende Zozibini
Tunzi (26) baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya Miss Universe
yaliyofanyika Atlanta, Georgia Kwenye studio za Tyler Perry.
Zozibini Tunzi amefanikiwa kutwaa Taji hilo
ambalo lilikuwa linashikiliwa na Catriona Gray Kutoka Ufilipino.
Mara ya mwisho kwa Afrika Kusini kushinda Taji
hili ilikuwa mwaka 1978 na mara ya pili ni mwaka 2017.
No comments:
Post a Comment
nice