Mkurugenzi
wa Clouds Media Group Joseph Kusaga amezindua kampeni ya ‘Bonge la Mpambanaji’ ambayo
ni maalum kwa ajili ya kuwawezesha Wahudumu wa Afya Tanzania kwa vifaa tiba na
mahitaji mengine kwenye vita hii dhidi ya kirusi corona.
Wakati akihojiwa
na Power Breakfast ya Clouds FM Kusaga
akasema anao Wapambanaji wenzake ambao
wako tayari kuungana na yeye na miongoni mwao ni Vodacom, Tigo na Diamond Platnumz
ambaye alimpigia simu ‘LIVE’ na kuzungumza kwenye Power Breakfast.
Akiongea
kwenye ‘PB’ Diamond alisema “Kwanza nimpongeze C.E.O Kusaga kwa kuweka nguvu
zake kwenye hilo sio kila Mtu mwenye moyo huo, mimi pia nitaweka mchango wangu
hapo na kama unavyofahamu tayari pia upande wangu nimeanza kulipia kodi familia
zilizokwama kutokana na hii corona”
Baada ya
kuzungumzia Bonge la Mpambanaji, CEO Kusaga alimtaka Diamond achague wimbo wake
ili uchezwe kwenye PB kuwaamsha Wapambanaji wote ambapo mara ya kwanza
alipendekeza apigwe msanii wake mpya zuchu lakini baada ya mkurugezi huyo kusisitiza kuwa ngoma ya Diamond ndiyo
inatakiwa, Platnumz alichagua yope remix na ikapigwa via Clouds FM kupitia
kipindi cha Power Breakfast
Hata hivyo
hali hii imekuja kwa tofauti sana kwa baadhi ya mashabiki ambapo baadhi yao walitoa
maoni yao juu ya msanii huyo kuunga mkono katika kampeni hiyo.
“Hiki kitu
binafsi nakitamani maisha yangu yote,natamani isiwe leo tu i wish siku zote
ngoma za wasafi zipigwe Clouds,hata kama kuna makando makando mengine huu ni
wakati wa ushirikiano kati ya Wasafi na Clouds fm,hivi mushawai kuwaza kama
kuna vitu vitafanyika kwa ushrikiano kati hizi kampuni 2 hapa bongo kuna moto
mkubwa sana utawaka kwenye tasnia hiyo?” aliandika moja ya mashabiki.
ROSE NDAUKA AWAJIBU WATU HAYA
Kupitia
ukurasa wake wa Instagram ameweka wazi jambo hilo kwa kuwata watu waache kujifanya kuwa wanajua
mambo mengi kuliko uhalisia wenyewe
“Maswali
yamekuwa mengi sana kuhusu kubadili dini, haya ni hivi nimetoka kwenye tumbo la
mwanamke wa kiislam na kulelewa na mwanamke huyu kwakifupi nimekuwa kwenye Uislam
na baba akiwa christian, Naveen ni Muslim kabisaaaa bila kupepesa sasa jamaniii
acheni kutaka kujua sana mengine tuwaachieni wenyewe,” aliandika Rose Ndauka.
Hili
limekuja mara baada ya Rose Ndauka kufunga ndoa ya Kiislam hivi karibuni na
mchumba wake wa siku nyingi ikiwa ni miezi michache tangu kuvishwa pete ya
uchumba.
DAVIDO
AWATOLEA POVU MASHABIKI WA WIZKID
Msanii
kutoka nchini Nigeria David Adedeji Adeleke ‘Davido’ ameonesha kuchukizwa na mashabiki wa Wizkid, awajia juu
hii ni baada yakuweka wazi ujio wa Kolabo yake na Nicki Minaj.
Kupitia
twitter, mashabiki hao kindakindaki wa Wizkid walianza kumbeza Davido kwa
kumwambia "Kama ingekuwa Wizkid, basi Nicki Minaj ndio angekuwa na wenge
la ku-tweet kuhusu hii Kolabo na kuitangaza, lakini sio kama ambavyo Davido
amefanya. OBO inatakiwa awe mpole." aliandika shabiki mmoja wa Wizkid.
Baada ya
hapo haikumchukua hata dakika Davido ambaye aliibuka na kujibu tweet hiyo kwa
kusema ana mpenda Wizkid na kumalizia na matusi mazito.
Mpenzi wa msanii wa Bongo Fleva Baraka Da Prince, Najdattani
amtetea mpenzi wake huyo kwakile kinachodaiwa kuwa anaongoza kuwajibu vibaya mashabiki
kupitia mtandao wa Instagram.
Akilifafanua
suala hilo Naj alisema kuwa sasa hivi amejitafuta na amebadilika kwa kutowajibu
watu vibaya katika mtandao wa Instagram.
“Kiukweli amelifanyia
kazi hilo jambo, sidhani kama kipindi cha hapa karibuni amemjibu mtu vibaya
kuna muda inatokea kama binadamu, kuna comments zinakukwaza sana hadi ukapoteza
muelekeo, huyu sio Barakah yule ambaye mmemzoea kwamba kila kitu kinamkasirisha
ndiyo maana amejitafuta kwenye hiyo miaka miwili". Alisema Baraka
Ikumbukwe
kwamba hili limekuja mara baada ya kuwepo kwa taarifa juu ya kutajwa kuwa mpenzi wake huyo
ndiye msanii anayeongoza kuwajibu vibaya
mashabiki mitandaoni.
No comments:
Post a Comment
nice