AFC Leopards ndiyo timu ya kwanza ya Kenya kufuzu nusu fainali baada
ya kuishinda Singida United na itacheza na Yanga hatua ya nusu fainali.
Gor
Mahia imefuzu baada ya kuitwanga Jang'ombe Boys ya Zanzibar kwa mabao
2-0 katika mchezo wa robo fainali uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru
jijini Dar.
Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere
ndiye mfungaji wa mabao yote mawili katika dakika ya 66 na 78. Sasa Gor
Mahia wanasubiri mshindi kati ya Simba dhidi ya Nakuru All Stars ya
Kenya pia ambao umeanza tayari.
No comments:
Post a Comment
nice