Utumiaji wa mihadarati bado ni mtambuka licha ya serikali katika
mataifa mbalimbali kuchukua hatu madhubuti ya kutokomeza utumiaji huo ambao kwa
asilimia kubwa umesababisha athali kubwa kwa baadhi watu hususani kwa vijana
ambao ndio waathilika wakubwa.
Vyazo mbalimbali vya habari ikiwemo tafiti ambazo
zimefanyika hivi karibuni zimeweza kufafanua jambo hili ambalo bado linaendelea
kushika kasi katika sehemu mbalimbali dunia
Kwa mujibu wa
shirika la Routers dawa aina ya heloini
imeongezeka kwenye pwani ya Kenya katika miaka ya hivi karibuni ikisemekana
kuwa dawa hizo zinatoka mara nyingi Afghanistan
zikipitishwa Mombasa kuelekea mataifa ya Magharibi hii ni kulingana na ripoti iliyotolewa hivi karibuni
na umoja wa Ulaya.
Miji ya Mobasa,Malindi na Ramu imeonekana kuathilika
zaidi hata hivyo mihadarati hiyo inapenya zaidi hadi kwenye miji mikuu
kama Nairobi hii ni kutokana na wingi wa
matumizi pia uwezo wa kifedha wa wanaoishi hapo.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa baadhi ya watumiaji wa
mihadarati wametengwa na jamii zao,mjini Mombasa baadhi ya washukiwa wa
matumizi ya dawa za kulevya wameshambuliwa hata kufika hatu ya kuchomwa
vilevile kuawa na haraiki ya watu ,
Hata hivyo imeleta picha mbaya sana kwa kuathili
shunguli za kitalii nchini Kenya. Utafiti zaidi uiliweka wazi kuwa sababu kubwa
ambayo inapelekea utumiaji wa dawa hizo ni ukosefu wa ajira kwa miongoni mwa
vijana waishio eneo hilo.
Hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwemo mijadara kwenye
Bunge, uhamasisho wa kijamii pamoja na ukamataji wa ulanguzi na kuchomwa kwa
dawa zinazopatikana ingawa hali
inaonekana kuzolota licha ya juhudi zote hizo.
Kwamujibu wa mtandao wa Tai unaeleza kuwa nchini
Tanzania matumizi ya dawa ya kulevya yameshuhudiwa miongoni mwa vijana ingawa
hatua madhubuti zimechukuliwa kwenye
vita dhidi ya tatizo hilo,Tume yakudhibiti mihadarati mijini Dar Es Salaam 2011 ilitoa
lipoti kuwa idadi ya watumiaji ilikuwa 1050 lakini hadi miaka ya hivi karibuni
imepanda zaidi ya nusu milioni.
Baadhi ya madhara yanayosemekana ni uharifu,
magonjwa ya zinaa ajali za barabarani na mauji kutokana na matumizi ya dawa za
kulevya.Mihadarati ambayo inatumika sana nchini Tanzania ni kama vile
bangi,cats, heroini na kokeini. Hata hivyo katika siku za hivi karibuni idadi ya
watumiaji inasemekana kupungua nchini Tanzania ikilinganishwa na Kenya.
Fayazani Mohamed ni moja ya aliyekuwa mtumiaji wa
dawa hizo hapa anaeleza namna ilivyokuwa ngumu kwake kuacha pia alivyonza
kutumia
“Nikijisemeye mimi mwenyewe ni hatua ngumu sana ya
kusema nimechoka lakini niliweza kushauliwa, kuambiwa na dungu jamaa kwamba
nisitumie kulingana nilikuwa nimechoka sana kiafya”. Fayazani Mohamed alisema.
Namna ambavyo alianza kutumia Fayazani alisema kuwa
kulingana na uwezo wa fedha aliokuwa nao pia marafiki wabaya ndio ilikuwa
chanzo cha kutumia matumizi ya dawa hizo, katika hatua ya kwanza mtu anajisikia
raha sana ambapo inasababisha matumizi kuongezeka kwa kila siku .
Pia Ally Masito ni moja ya aliyekuwa mtumiaji wa
dawa ambapo mpaka sasa ana miaka sita akiwa hatumii anasemakuwa yeye kwa upande
wake kilichosababisha kutumia dawa hizo ni mahusino ya kimapenzi ambapo
alimpenda binti kwa baadaye wazazi wa msichana huyo walikataa uhusiano huo na
hapo akawa ni mtu wa mawazo mengi na ndipo akaona furaha kubwa ni kutumia dawa
hizo ingawa bado iliendelea kumtesa kwasababu alijikuta akianza tabia ya wizi
na unyanganyi kitendo ambazo kilizidi
kumtesa sana .
Taibu Abdul Rahmani ni mwanaharakari na mwanasaikologia
pia mshauri akiwa pwani ya Kenya anasema kuwa tatizo hili ni kubwa sana
ukiangalia hasa katika mwambao wa pwani tumeadhiliki pa kubwa sana na hili ni
jambo ambalo lilitokea katika familia yetu na niliweza kupoteza mkubwa wangu
katika janga la dawa za kulevya na ndiyo ikwa ni msukumo kuingia na kusaidia wengine katika hali ambayo
wanawezo kurudi kuwa sawa.
Kitu ambacho kinapelekea mtu kutumia dawa hizo
zinakuja kwa njia nyingi sana ukiangalia suala la heroini ambao ndio unga
utumiaji wake unahitaji kwa mara tatu kwa mtuamiaji sungu kwahivyo lazima uwe
na ile chanzo cha wewe kuanza kutumia katika pwani Kenya ukiangalia Mombasa mpaka Ramu elimu hakuna.
Kwahiyo katika jamii ya watu wanapokulia kuna muda
fulani ambao tunakosea katika maisha kitu ambacho kinasababisha kuzama katika
mambo kama haya pia matumizi ya dawa mengine ni kama vile bangi, mirungi,pombe
ni baadhi ya vitu vinavyomsukumu mtu kuingia katika uraibu wa unga,
Athali zake ni kubwa sana moja wapo ni
yakisaikolojia mtu anaathilika kwasababu kila siku anataka kutumia ili aishi
vilevile afya yake inazolota kwasababu muda wote hufikilia kupata dawa kila
siku.
Hata hivyo Agata Mbale alitoa mtazamo wake huku
akipinga tabia ya watu kujihusisha katika tabia hiyo ambayo ni hatal “napinga
sana kitu kiitwacho mihadarati kwasababu
husababisha vijina wengi kutoka na kuingia kwenya mambo mabaya ambayo ni maovu
kutokana na kutumia mihadarati.
Mihadarati inakuwa mitaani watu wanaitumia
wanaapotoka hasa hasa kwa vijana wengi wanashindwa kufanya kazi kwa kuendekeza
mambo siyo ya msingi halafu mwisho wa siku wanakuja wanasema wanajuta.
Kwahiyo napenda kuwambia vijana wenzangu utumiaji wa
mihadarati ni mbaya sana inatakiwa tuikwepe ili tufanye kazi kwa bidii kwa
sababu vijana ni nguvu ya Taifa”; .Agata Mbale
kutoka Mrongoro Tanzainia.
Katika hali ambayo siyo ya kawaida baadhi ya watumiaji
ambao wanashindwa kupanda dawa hizo wanatumia dawa ya panya, mafuta ya petrol na
vingine vingi kwa ajili ya kujiridhisha.
Hivyo serikali katika mataifa mbalimbali bado
inahitaji kuongeza juhudi katika kupambana na kutokomeza tatizo hili ambalo
bado ni mtambuka.
No comments:
Post a Comment
nice